Перейти к содержимому

#MAHUBIRI MUNGU HUTOA KWA WAKATI UNAOSTAHILI, WAUMINI WATAKIWA KUTIMIZA NADHIRI - LANGENIONE

KANISA LA MORAVIAN KIGAMBONI

0:00 / 0:00

#MAHUBIRI MUNGU HUTOA KWA WAKATI UNAOSTAHILI, WAUMINI WATAKIWA KUTIMIZA NADHIRI - LANGENIONE

51 просмотр · 2 недели назад
KANISA LA MORAVIAN KIGAMBONI
324 подписчика
51 просмотр · 2 недели назад
#MAHUBIRI Mtumishi wa Mungu Langenione Kibona amewataka waumini kuwa na imani kwa Mungu na kuelewa kuwa si kila wanachokiomba hupewa kwa wakati wanaoutaka, bali Mungu hujua mahitaji na wakati sahihi wa kuwapatia. Amesema wakati mwingine mtu anaweza kuomba jambo kubwa, lakini akawa hana uwezo wa kulisimamia, hivyo Mungu huandaa kwanza mtu huyo kabla ya kumpa kile anachokihitaji. Akihubiri katika Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Kigamboni, Kibona amesema waumini wanapaswa kutanguliza kutafuta Ufalme wa Mungu na haki yake, akirejea Mathayo 6:33 inayosisitiza kuwa wanapotanguliza Ufalme wa Mungu, mahitaji yao yatazidishwa. Amesema waumini wanapotoa kwa ajili ya kazi ya Mungu wanapaswa kufanya hivyo kwa moyo wa dhati na kuendelea kumtumainia Mungu. Aidha, Mtumishi huyo amesisitiza umuhimu wa kutimiza nadhiri na ahadi zinazowekwa mbele za Mungu, akieleza kuwa mtu akiahidi jambo kwa Mungu anapaswa kulitekeleza. Akitolea mfano wa Yeftha katika Waamuzi 11:30–40, amesema nadhiri si jambo la kuahidi kwa wepesi, bali linahitaji uwajibikaji na utekelezaji, huku akiwataka wale ambao hawajatimiza nadhiri zao kutubu na kisha kutekeleza walichoahidi.