MAKONDA ATEMA POVU "JEZI NI MBAYA, KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA"
ITV Tanzania
0:00 / 0:00
MAKONDA ATEMA POVU "JEZI NI MBAYA, KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA"
620 просмотров · 19 часов назад
ITV Tanzania
1,37 млн подписчиков
620 просмотров · 19 часов назад
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Timu ya Taifa, Taifa Stars, ni mali ya Nchi na si kampuni ya mtu binafsi, akisisitiza kuwa mamlaka ya Waziri katika kusimamia sekta ya michezo yanatokana na Sheria, Sera na Kanuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Makonda amesema: “Timu ya Taifa ni mali ya Nchi, sio kampuni ya Mtu, ndiyo maana tumeikasimu na kuihudumia, timu ikienda popote pale, ni Nchi inaenda.”
Makonda pia amesema: “Wanamfanya kama Waziri wanamdharau, lakini huyo ni mteule wa Rais anayesimamia wizara ambayo inakupa mkate.” Kauli hiyo inakuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu mamlaka na usimamizi wa Timu za Taifa, hususan baada ya mvutano kuhusu jezi mpya za Taifa Stars.
“Ninapozunguka huko duniani naona viwango na mimi natamani wageni wakija kwetu wakute kuna viwango…mtu mmoja akanambia jezi hizi wewe umeziona nikamwambia nimeziona kwenye picha, akisema sasa usizione laivu, picha zimesafishwa...” Paul Makonda – Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ;
Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3
Twitter : https://bit.ly/2XG7aii
Instagram : https://bit.ly/34KItmg