Перейти к содержимому

POINTI 15 ZA DEREVA : MASHINE ZIKATE, SIO ASKARI || ASKARI WAANDIKA FAINI NA KULIPA WENYEWE

CHAWAMATA TV

0:00 / 0:00

POINTI 15 ZA DEREVA : MASHINE ZIKATE, SIO ASKARI || ASKARI WAANDIKA FAINI NA KULIPA WENYEWE

9 348 просмотров · 9 часов назад
CHAWAMATA TV
31,1 тыс. подписчиков
9 348 просмотров · 9 часов назад
DEREVA MSOMI - ASIMULIA MKASA Dereva Rajab Rashid amefika katika ofisi za Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania (CHAWAMATA) kutoa malalamiko kuhusu changamoto anazodai kukutana nazo katika utekelezaji wa kazi yake ya udereva. Rajab amesema alikamatwa eneo la Hans Seketwa, Songwe, baada ya askari wa usalama barabarani kumzuia kwa madai ya kuendesha kwa mwendo wa kasi wa kilomita 59 kwa saa. Anadai aliomba kuonyeshwa ushahidi wa kamera uliothibitisha kosa hilo, lakini hakuridhishwa na maelezo aliyoyapata. Kwa mujibu wa maelezo yake, alifika kituoni kufuatilia suala hilo na kudaiwa kuwa askari waliokuwa wamemwandikia hati hiyo walikuwa wamekosea. Pia amesema alitaka kupewa risiti baada ya kulipa, lakini hakupatiwa. Dereva huyo amesema amekuwa akiendesha magari kwa takribani miaka 28 na anataka mifumo ya kamera itumike katika kubaini makosa ya madereva, badala ya maamuzi yanayoweza kuleta malalamiko au kutokuelewana. Aidha, Rajab amezungumzia mfumo wa pointi kwenye leseni za madereva, akisisitiza kuwa mashine na kamera zitumike pale inapowezekana kuthibitisha makosa kama mwendo kasi na kutofunga mkanda. Ameomba mamlaka husika kuhakikisha haki inatendeka na madereva wanapata nafasi ya kuthibitisha makosa wanayodaiwa kufanya. *Tazama mahojiano yote ya Dereva Rajab Ab Rashid kupitia CHAWAMATA TV ONLINE.* #CHAWAMATA #CHAWAMATATV #Madereva #MaderevaWaMalori #Dereva #UsalamaBarabarani #PointSystem #PointiZaLeseni #Songwe #Mbeya #Tunduma #UsalamaBarabarani #Malalamiko #HakiZaMadereva #TruckDrivers #TruckDriversTanzania #Tanzania #Habari #CHAWAMATAONLINE