Kujifungua ni wiki ngapi?
ULY CLINIC
0:00 / 0:00
Kujifungua ni wiki ngapi?
8 199 просмотров · 4 г. назад
ULY CLINIC
12,3 тыс. подписчиков
8 199 просмотров · 4 г. назад
Inakadiliwa kuwa binadamu hubeba ujauzito kwa wastani wa muda wa wiki 40 kamili. Makadilio haya si kila mwanamke huyafikia, hii ndio maana baadhi hujifungua chini ya wiki hizi 40, na wengine hujifungua baada ya wiki 40 kupita
Wiki ngapi ni salama kujifungua?
Kujifungua huwa salama endapo itatokea wakati kichanga amekomaa
Tafiti zinaonyesha kuwa ujauzito hukamilika unapofikisha wiki 37 mpaka 42
Kujifungua kwenye kipindi hiki huwa na maudhi kidogo kwa kichanga
Wakati kujifungua kabla au baada ya wiki 37 hadi 42 huambatana na maudhi makubwa kwa kichanga na mama
Tarehe ya matazamio ya kujifungua
Tarehe ya matazamio ya kujifungua Hukokotolewa kwa kuzingatia nadharia ya kwamba kipindi kamili cha ujauzito ni wiki 40
Asilimia 4 tu ya wanawake hujifungua katika tarehe zao za matazamio
Asilimia 86 ya wanawake waliobaki hujifungua kabla ya tarehe ya matarajio ya kujifunguaa
Na asilimia 10 ya wajawazito waliobaki hujifungua baada ya wiki 42 kupita
Wakati gani utasemekana umewahi kujifungua?
Endapo utajifungua ujauzito ukiwa na wiki chini ya 37, itasemekana umejifungua kabla ya wakati
Kujifungua kabla ya wakati kumegawanyika katika makundi pia
Madhara ya kujifungua kabla ya wakati
Baadhi ya madhara yanayowezaa ambatana na kujifungua kabla ya wakati ni
Kujifungua mtoto njiti au uzito mdogo kupita kiasi
Kujifungua baada ya wakati
Ni kujifungua baada ya wiki 42 za ujauzito yaani siku 294 kupita
Madhara ya kujifungua baada ya wakati
Kujifungua kwa kuanzishiwa uchungu
Kujifungua kwa upasuaji
Mtoto kufia tumboni au kufa baada ya kujifungua
Mtoto kuzaliwa na uzito mkubwa
Kichanga kuvuta kinyesi
Mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua
Kujifungua kwa shida
Majeraha kwenye mlango wa uzazi na Kuchanika msamba
Kupata maambukizi ukeni au kwenye kizazi baada ya kujifungua
Kuishiwa damu
Kama ujauzito wako umepitiliza umri, au unapata dalili za uchungu kabla ya wakati
Wasiliana na daktari wako kwa msaada Zaidi
Subscribe channel yetu ya ULY CLINIC-youtube kwa video na Makala mpya za afya
Asante kwa kutazama