Перейти к содержимому

Maulidi ya Sheikh Salum Lodi - Oysterbay

Shadhuly East & Central Africa

0:00 / 0:00

Maulidi ya Sheikh Salum Lodi - Oysterbay

4 682 просмотра · 5 лет назад
Shadhuly East & Central Africa
6,26 тыс. подписчиков
4 682 просмотра · 5 лет назад
Matukio Muhimu 00:00 Laylaha illah llah - qaswida kutoka madrasat shadhuly 08:27 Maulid Mlango wa Kwanza 11:11 Nyoyo zimefurahika - Seyyid Bahsaan Abdillah 17:16 Subuhul Hudaa - Qaswida Kutoka Madrasat shadhuly 22:06 Qiyaam kutoka Madrasat shadhuly 24:47 Yaa Habibi ya Muhammad - Shadhuly Qaswida 27:33 Mlango wa Maulid - Masjid Mtoro Wasifu wa Sheikh Salum Lodi ALIVOISHI NA MASHEIKH NA WANAZUONI. 🎈Nae Sheikh Khamis Mataka ..pale Masjid Manyema huku akiwa na huzuni na majonzi tele huku chozi likimtiririka ..alijitahidi kumuelezea Shk Salim na jinsi walivyoshirikiana vyema katika Taasisi ya Wanazuoni...maarufu Jopo la Masheikh .. ..anasema Shk Mataka kwamba JOPO..linaendesha kazi zake kwa kutegemea michango ya Wana Jopo wenyewe...na hapa ndipo Shk Salim alipoweza kuonesha Ukarimu wake ..kwa kutoa michango mingi ktk Kuendesha harakati na vikao mbalimbali vya Jopo kwa muda wote wa umri wake toka lilipoanzishwa Jopo hilo...Sheikh Mataka alikwenda mbali ..zaidi ..akaeleza hata fenicha zote za Ofisi ya Jopo zenye thamani ya shilingi takriban milioni sabiini...zote alitoa Shk Salim Lodi..na walipotaka kufanya mchakato wa kumfidia japo baadhi yake...Sheikh Salim alikataa .. 🎈Muft atoa siri.... Hapo hapo Manyema ..Muft Alhabib Shk Abubakar Zuber nae ktk kumueleza Shk Salim..hatimae akatoa siri kwamba Shk Salim alikuwa ni mshauri wake wa karibu sana ktk mambo mengi.... 🎈Kichangani Wanalia..Masjid Kichangani ambako ndio sehemu ambayo Shk Salim Lodi...kama ni mbawa ..basi huko ndiko alipochanua mbawa zake zote... 🎈Alipopewa nafasi tena Shk Walid Kuzungumza ktk Khitma .Masjid Maamur....alizidisha zaidi.kutoa khutba fupi yenye ujumbe mzito sana na wenye mazingatio makubwa sana kwa kila mwenye akili timamu... ... 🎈Shk Walid alimalizia kwa kumsifu Shk Salim kwamba alikua na mpango madhubuti na endelevu wa kujitayarisha na safari ya Akhera...akakumbuka jinsi alivyomuweka kua Imam pale Masjid Kichangani na alivyomshauri aachane na kuulamba kuvaa shati na suruwali...na kumpa kanzu ili aanze kuvaa kanzu...pia alikumbuka jinsi alivyomtuma atembee ...Magomeni yote...Kagera..Mikumi. .Makanya ..Mapipa..Mwembe Chai nk...akaangalie kuna madrasa ngapi na kuna walimu wangapi na mahitaji yao ni nini... Na alipoletewa jibu .Shk Salim akawa anawalipa posho Walimu takriban 48 wa madarasa .yaliyohakikiwa kutoka madrasa zaidi ya 193...kwa zaidi ya miaka 10 Shk Walid pia alidokeza kwamba Shk Salim..alikua akitoa Daku pale Masjid Kichangani wakati wa mkesha..kwa takriban miaka 15.mfululuzo.... 🎈Masjid Shadhilly..ambako ndipo Shughuli za mazishi zilipofanyika...tulisikia mambo mengi jinsi Shk Salim alivyoweza kuzikonga nyoyo za mabwana wakubwa Masharifu..Masheikh na wanazuoni mbalimbali...kama tulivyotaja ktk sehemu zilizopita.. .Kwa leo tutamalizia kwa maneno ya Shk Walid pale Masjid Maamur..aliponukuu.... ..Sote ni wasafiri na chombo chetu tunachosafiria ni uhai.pumzi tulizonazo..kila siku tukilalala na kuamka ndivyo tunavyopiga khatua kuelekea Akhera... 🎈Alikuwa Karimu sana... Tabia yake hii ..ya ukarimu ilikuwa kama smaku inayozinasa nyoyo za maelfu ya watu aliojuana nao na ambao hakujuana nao..bali wao walimjua .... Huwezi kwenda kwa Shk Salim Lodi kwa shida yoyote na ukarudi patupu ..lazima utatabasamu tu .. Mkono wake ulikua mwepesi Alikuwa akiwasaidia watu wa rika zote bila ubaguzi wa aina yoyote...