Перейти к содержимому

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - SIKU YA KUSIFU NA KUABUDU | 06 SEPTEMBER 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

0:00 / 0:00

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - SIKU YA KUSIFU NA KUABUDU | 06 SEPTEMBER 2026

18 357 просмотров · Трансляция закончилась 2 дня назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
64 тыс. подписчиков
18 357 просмотров · Трансляция закончилась 2 дня назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - SIKU YA KUSIFU, KUABUDU PAMOJA NA UTOAJI WA FUNGU LA KUMI| 06 SEPTEMBER 2026 UJUMBE WA LEO: MUNGU NA MALI (GOD AND WEALTH) Luka 16 : 1 - 13 1 Tena, aliwaambia wanafunzi wake, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. 2 Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena. 3 Yule wakili akasema moyoni mwake, Nifanyeje? Maana, bwana wangu ananiondolea uwakili. Kulima, siwezi; kuomba, naona haya. 4 Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao. 5 Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? 6 Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. 7 Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini. 8 Yule bwana akamsifu wakili dhalimu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru. 9 Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele. 10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. 11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? 12 Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. (Kumbukumbu 8:1-20, Kumbukumbu 8:1-20) HOJA ZA MSINGI ZA KIFALSAFA NA KITHEOLOJIA: 1. KATIKA BIBLIA HOJA TATA KABISA NA MANENO YENYE UTATA NA FALSAFA NGUMU KABISA AMBAYO YESU ALIWAHI KUSEMA NDIYO SOMO LA LEO..." HAMWEZI KUMTUMIKIA MUNGU NA MALI"...Luka 16:13 HAYA NI MANENO MAGUMU KABISA AMBAYO YESU MWENYEWE ALIWAHI KUSEMA. HII NI FALSAFA NGUMU AMBAYO YESU MWENYEWE ALISEMA: 2. MADHARA YA FALSAFA HII NI KUBWA KAMA HAIKUTAFSIRIWA VIZURI NA KWA USAHIHI INAWEZA KULETA MGAWANYIKO WA MAKUNDI YA WATU. 》WENGINE WANAWEZA KUACHA KAZI NA KUJITENGA NA UCHUMI NA KUISHI KWENYE UMASIKINI MKUBWA NA MAISHA YA MATESO. 》WENGINE WENYE MALI NA HALI NZURI YA KIUCHUMI WANAWEZA KUISHI KWENYE MSONGO NA KUAMINI MUNGU AMEWAACHA BAADA YA KUBARIKIWA KWAO NA KUWA NA MALI NA UMILIKI WA VITU NI KAMA UASI 3. MUNGU NA MALI (GOD & WEALTH) 》KITABU CHA KUMBUKUMBU LA TORATI MLANGO MZIMA WA NANE UNATHIBITISHA WAZI.".... MUNGU NDIYE AKUPAYE NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI, MALI, WEALTH..." 》MUNGU HUVUNJA MALANGO YA SHABA NA MAPINGO YA CHUMA NA KUKUPA MALI ZILIZOFICHWA MAHALI PA SIRI (Isaya 45:2-3) 1. MUNGU ALIMPA ADAMU NA HAWA MALI 2. MUNGU ALIMPA IBRAHIMU MALI 3. MUNGU ALIMPA ISAKA MALI KIPIMO KIMOJA KWA MIA ....AKAWA TAJIRI KULIKO SERIKALI (Mwanzo 26:12-17) 4. MUNGU ALIMPA YAKOBO MALI 5. MUNGU ALIMPA YUSUFU MALI KIASI CHA KULISHA DUNIA 6. MUNGU ALIMPA SULEMANI MALI NYINGI 7. MUNGU AMELIPA KANISA MALI NYINGI NA KUMILIKI MUDA WA DUNIA 4. SHIDA NI KUTANGULIZA MALI MBELE NA KUIPA MALI KIPAUMBELE KULIKO MUNGU. 》KUMBUKUMBU LA TORATI MLANGO MZIMA WA 28 UNAELEZA KWA WAZI. 》MUNGU ANATOA MAONYO YA KIBURI CHA MALI NA KUJISIFU KWA MWANADAMU KAMA NEBUKADREZA MFALME WA BABELI SIKU ZILE ALIPELEKWA PORINI NA KUKAA HUKO MIAKA SABA. 》KITABU KIZIMA CHA WAAMUZI KINAELEZEA KWA WAZI PALE ISRAEL WALIPOMUACHA MUNGU WALIPITIA NYAKATI NGUMU ZA KIUCHUMI NA NJAA KIASI CHA KULA NYAMA ZA WATOTO NA KULA MAVI YA NJIWA. VIPI KUHUSU NCHI YAKO KULIWA NA WAGENI?? (Kumbukumbu 28:33, Yeremia 5:15-17) NI TAIFA GANI LA KIGENI LIMEVAMIA AFRIKA KWA NGUVU YA KIUCHUMI, KIBIASHARA NA KIFEDHA KWA MITAJI MIKUBWA INAYOUWA MITAJI MIDOGO YA WANANCHI?? VIPI KUHUSU SIFA YA WAKILI DHALIMU. HIVI HAWA NI WAWEKEZAJI AU WAKILI DHALIMU ? "...KWA KUWA WANA WA ULIMWENGU HUU KATIKA KIZAZI CHAO WENYEWE HUWA NA BUSARA KULIKO WANA WA NURU..." Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com