TANROADS YABORESHA MABANGO YA MAELEKEZO DAR, MADEREVA WAPONGEZA
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
TANROADS YABORESHA MABANGO YA MAELEKEZO DAR, MADEREVA WAPONGEZA
6 599 просмотров · 7 дн. назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
6 599 просмотров · 7 дн. назад
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kuboresha na kufunga mabango mapya ya maelekezo katika maeneo mbalimbali ya jiji, hatua ambayo imepongezwa na madereva wakisema itarahisisha utambuzi wa maeneo na mwelekeo kwa watumiaji wa barabara.
Mabango hayo mapya yenye ukubwa na urefu zaidi yameanza kuonekana katika baadhi ya barabara na makutano, yakionyesha majina ya maeneo pamoja na mwelekeo wa kwenda katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Lazeck Kyamba, amesema mabango hayo yamewekwa baada ya kubaini kuwa baadhi ya yaliyokuwepo yalikuwa yamechakaa au kuharibika baada ya kugongwa, huku mengine yakiwa madogo kiasi cha kutokuonekana kwa urahisi.
“Mabango haya yana herufi kubwa sana na yanaonyesha direction ya wapi unakwenda. Mengi yalikuwa yamegongwa lakini mengine yalikuwa machakavu. Sasa tunayarudisha, tunaanza kuyafunga na kuyaboresha zaidi,” amesema Kyamba.
Amesema ukubwa na urefu wa mabango hayo umezingatia pia changamoto ya uwepo wa malori mengi katika baadhi ya barabara, hali inayoweza kuzuia mwonekano wa mabango kwa madereva wanaokuwa nyuma ya magari makubwa.
“Kwa sababu ile barabara ina malori mengi, mtu akiwa nyuma ya lori na bango likawa halina urefu wa kutosha, anaweza asione bango la mbele kwa sababu amekingwa na lori,” amesema.
Kwa mujibu wa Kyamba, TANROADS imeanza mpango huo katika barabara zinazoelekea Uwanja wa Ndege na itaendelea na ufungaji wa mabango hayo katika makutano mbalimbali ya barabara jijini Dar es Salaam.
Amesema lengo ni kuhakikisha dereva anapofika katika makutano anapata taarifa kwa wakati kuhusu eneo alilopo na mwelekeo wa anakoelekea