
Идёт прямой эфир
Трансляции Youvio пока не открывает — они идут другим способом доставки, чем обычные видео. Записи завершённых эфиров и остальные ролики работают как всегда.
DCI KINGAI AREJEA NCHINI, LISSU ATAKA KUKUTANA NAYE KABLA YA KIZIMBANI, ATOA TAMKO ZITO |
В эфиреСейчас смотрят: 458 · Трансляция началась 2 часа назад
HARAKATI TV
96,7 тыс. подписчиков
Сейчас смотрят: 458 · Трансляция началась 2 часа назад
DCI KINGAI AREJEA NCHINI, LISSU ATAKA KUKUTANA NAYE KABLA YA KIZIMBANI, ATOA TAMKO ZITO |
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, imeingia katika hatua mpya baada ya shahidi wa tano wa upande wa utetezi, John Heche, kukamilisha ushahidi wake.
Baada ya Heche kumaliza ushahidi, matarajio yalikuwa kwamba mmoja kati ya mashahidi watatu wa Lissu — Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camillius Wambura na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai — angeanza kutoa ushahidi.
Hata hivyo, mashahidi hao hawakuwapo mahakamani, hali iliyosababisha kesi kuahirishwa hadi Ijumaa, Septemba 18, 2026.
Katika video hii tunachambua kwa kina kilichotokea Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kwanini mashahidi hao wamekuwa sehemu muhimu ya hatua inayofuata ya kesi, na kwa nini Tundu Lissu ameomba apewe nafasi ya kukutana nao kabla ya kutoa ushahidi.
Lissu amesema anataka kujadiliana na mashahidi hao kuhusu ushahidi watakaoutoa, huku DCI Ramadhani Kingai akitajwa kuwa anatarajiwa kufika mahakamani Ijumaa. Kwa upande mwingine, bado haijajulikana CDF Jenerali Jacob Mkunda na IGP Camillius Wambura watarudi lini nchini.
Upande wa Jamhuri umesema hauna pingamizi kuhusu kuahirishwa kwa kesi, lakini umeitaka Mahakama imsisitizie Lissu kuhakikisha mashahidi wake wanafika ili kesi iweze kuendelea.
Jaji Dunstan Ndunguru pia amesisitiza wajibu wa kila upande katika kesi hiyo, akirejea kauli kwamba Mahakama si mama wa upande wowote.
Tazama video hii hadi mwisho kwa uchambuzi wa kina kuhusu hatua hii ya kesi ya Tundu Lissu, mashahidi watatu wanaotarajiwa kutoa ushahidi na kinachoweza kufuatia katika hatua za mwisho za ushahidi wa utetezi.
Usisahau KU-SUBSCRIBE Harakati TV, kuwasha BELL na kushare video hii ili kupata taarifa, habari na uchambuzi zaidi kuhusu siasa, jamii na matukio mbalimbali Tanzania.
#TunduLissu #Lissu #Chadema #KesiYaLissu #Uhaini #DCIKingai #CDFMkunda #IGPWambura #JohnHeche #HarakatiTV #Tanzania