Dua bora ya kuomba msamaha kwa Allah
Uislamu Dini Ya Haqi
0:00 / 0:00
Dua bora ya kuomba msamaha kwa Allah
33 058 просмотров · 7 лет назад
Uislamu Dini Ya Haqi
749 подписчиков
33 058 просмотров · 7 лет назад
Miongoni mwa du’aa za kuomba maghfira, ni hii du’aa inayoitwa 'Sayyidul-Istighfaar' (Du’aa bora ya kuomba maghfira kupita zote) aliyotuusia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Du’aa ambayo ndani yake imekusanya maana zote za tawbah na kukiri, na kwamba hapana mwenye kusamehe makosa isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).
Imeposimuliwa kutoka kwa Shaddaad bin ‘Aws (Radhiya Allaahu ‘Anhu) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Bwana wa kuomba maghfira ni kusema:
اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لا إِلَهَ إلا أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلا أَنْتَ.
Allaahumma anta Rabbiy laa ilaaha illa Anta. Khalaqtaniy wa ana ‘abduka. Wa ana ‘alaa ‘ahadika wa wa’adika ma statwa’atu. A’udhu bika min sharri ma swana’atu. Abu-u laka bini’imatika ‘alayya wa abu-u laka bidhanbiy, faghfirliy, fainnahu laa yaghfiru dhunuuba illaa anta.
Akasema: Atakayesema hayo wakati wa mchana akiwa na yakini juu yake akafa siku hiyo kabla ya usiku kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi. Na atakayesema hayo wakati wa usiku akiwa na yakini juu yake akafa kabla ya asubuhi kuingia, huyo ni katika watu wa Peponi.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na wengine]