MELI YA MV LIEMBA YAANZA MAJARIBIO ZIWA TANGANYIKA, INAKIMBIA KINOMA- WAZIRI MBARAWA ASIMAMIA.
Kadi News24
0:00 / 0:00
MELI YA MV LIEMBA YAANZA MAJARIBIO ZIWA TANGANYIKA, INAKIMBIA KINOMA- WAZIRI MBARAWA ASIMAMIA.
6 398 просмотров · 1 месяц назад
Kadi News24
37,9 тыс. подписчиков
6 398 просмотров · 1 месяц назад
@wajinatv3033 @KadiNews @bintikigoma
KIGOMA.
Meli kongwe ya Mv Liemba iliyosimama kazi kwa zaidi ya miaka kumi, imeanza rasmi majaribia baada ya serikali kutumia bilioni 34 kufanya ukarabati na uwekezaji katika meli hiyo, ambapo inatarajiwa kuanza safari zake kwa nchi jirani za Burundi, Zambia na Congo DRC ifikapo September mosi mwaka huu.
Majaribio ya kuanza safari kwa meli ya Mv Liemba katika ziwa Tanganyika baada ya ukarabati, umesimamiwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, ambapo majaribio hayo ni awamu ya kwanza, kabla ya majaribio ya mwisho na kuanza safari zake.
Meli ya Mv Liemba inauwezo wa kubeba Abiria takribani 600 na mizigo tani 200, ambapo kulejea kwa usafirishaji wa kutumia Meli katika Ziwa Tanganyika, imeelezwa kuwa chachu ya kukuza mzunguko wa biashara hasa ikiwemo usafirishaji wa mizigo na abiria, na kuufungua mkoa wa Kigoma uchumi na kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni kutoka mataifa jiraji.
Waziri wa Uchukuzi Profesa Mbarawa, amepongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuchukua hatua ya kukarabati meli hiyo, ambapo ameelekeza mkandarasi kuhakikisha anakamilisha hatua zilizobaki, ili malengo ya kulejesha usafiri wa meli katika ziwa Tanganyika yaweze kutimia na kufungua milango ya kukuza uchumi.
MWISHO.