Перейти к содержимому

OVAH TANZANIA YATOA ELIMU YA UZAZI KWA VIJANA

Radiojamii Kilosa

0:00 / 0:00

OVAH TANZANIA YATOA ELIMU YA UZAZI KWA VIJANA

28 просмотров · 7 дн. назад
Radiojamii Kilosa
252 подписчика
28 просмотров · 7 дн. назад
Shirika lisilo la Kiserikali la OVAH Tanzania, kupitia Mradi wa SEMA NAMI, limetoa mafunzo kwa vijana wa Kata ya Magomeni, Wilaya ya Kilosa, yanayohusu afya ya uzazi, hedhi, balehe, jinsia, usawa na haki, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana kupata elimu na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. Akizungumza na Redio Jamii Kilosa, Mkurugenzi wa OVAH Tanzania, Bi. Modesta Joseph, amesema Mradi wa SEMA NAMI umefika Wilayani Kilosa kwa lengo la kuwapatia vijana elimu muhimu itakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya zao, hususan katika masuala ya afya ya uzazi, hedhi, balehe na afya ya akili. Bi. Joseph amesema elimu hiyo inalenga kuwawezesha vijana kufahamu haki zao, kutambua changamoto zinazoweza kujitokeza katika kipindi cha balehe na kujenga uelewa utakaowasaidia kujilinda dhidi ya changamoto mbalimbali za kiafya na kijamii. Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa SEMA NAMI Chatbot, unaowawezesha vijana kupata elimu na taarifa kuhusu afya na haki za uzazi pamoja na masuala ya jinsia kupitia simu janja. Mfumo huo unalenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa vijana na kuwapa fursa ya kupata elimu wanapohitaji.‪@ovahtanzania3119‬ ‪@Mwlkyombo‬ ‪@Mwlkyombo‬ ‪@millardayoTZA‬ ‪@SunUdaya‬