Перейти к содержимому

ORDINATION YA WANAWAKE KUAMURIWA KWA DARAJA TAKATIFU LA USHEMASI NA UKASISI

Rev.Can.Wilson Mafumbi

0:00 / 0:00

ORDINATION YA WANAWAKE KUAMURIWA KWA DARAJA TAKATIFU LA USHEMASI NA UKASISI

43 просмотра · 2 мес. назад
Rev.Can.Wilson Mafumbi
2,2 тыс. подписчиков
43 просмотра · 2 мес. назад
HISTORIA FUPI NA MCHAKATO WA WANAWAKE KUKUBALIWA KUAMURIWA KATIKA DARAJA TAKATIFU LA UKASISI NA USHEMASI KATIKA KANISA ANGLIKANA Na Revd.Canon Wilson Mafumbi , Hoja ya kuamuriwa kwa wanawake katika daraja la ushemasi na Ukasisi  siyo kwamba ni mara yake ya kwanza kuletwa  na kujadiliwa katika Kanisa Anglikana. Hoja hii imeshajadiliwa katika  Kanisa hapa duniani kwa ujumla wake, Kanisa la Anglikana Ulimwenguni limejadili kwa kina katika mikutano na makongamano yake mengi kwa siku nyingi. Ordination of women in the Anglican communion - (Primates' Meeting, Lambeth Conferences,  AnglicanConsultative Council  Bishops Meetings) The ordination of women has been a controversial issue throughout the Anglican Communion. By 2010, however, 28 of the 38 provinces of the Anglican Communion ordain women as priests and 17 have removed all barriers to women serving as bishops. Women take difficult journey into priesthood SINODI YA JIMBO Hoja ya kuamuriwa wanawake inahusu Imani na taratibu na kwa msingi huo ni hoja ambayo ilihitaji makabaliano ya Jimbo zima. Hivyo Sinodi ya kumi na moja ya  Jimbo iliyofanyika katika ukumbi wa CTC- CCT Dodoma tarehe 27 -29 Oktoba 1999, Katika agenda namba 25/1999 Katibu mkuu aliwasilisha agenda hii  ambayo ilikuwa ni mara ya pili kuletwa. Wajumbe walijadili hoja hiyo kwa nyumba na kisha  Sinodi ikatoa uamuzi au msimamo wa jimbo juu ya hoja hii. Taarifa ya nyumba, Nyumba ya Makasisi walikuwa 27 14 walisema hapana 11 walisema wakati bado 1 alikuwa neutral ( hakukataa wala kukubali 1 aliguna Nyumba ya walei Walisema kwa vile suala hili lina mgogoro Sinodi itamke , Madayosisi  yaliyotayari yaendelee na yale yasiyo tayari yaache. Nyumba ya Maaskofu  walikuwa 11 walisema walio wengi , Jimbo haliko tayari kuwawekea wanawake kuwa  mashemasi na makasisi. Hata hivyo kwa wale waliotayari waendelee isipokuwa uwekwe utaratibu wa kanuni za kufuatwa ili kutekeleza jambo hili. Maaskofu 5 walisema hapana Maaskofu 5 walisema wakati bado Askofu  1 alisema ndiyo TAMKO LA SINODI YA JIMBO   ( MSIMAMO WA KANISA ANGLIKANA  TANZANIA KUHUSU KUAMURIWA WANAWAKE KUWA WACHUNGAJI ) Kwa kuwa sehemu kubwa ya jimbo bado halijakubali kuamuru wanawake kuwa mashemasi na Makasisi, na kwa kuwa  kuna dayosisi iliyo tayari; SINODI INAAGIZA KWAMBA Dayosisi iliyo tayari inaweza kuwaamuru wanawake kuwa Makasisi na Mashemasi kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na nyumba ya Maaskofu. Tamko hili lilipigiwa kura,Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: Waliosema ndiyo      42 Waliosema hapaana   3 Wasio upande wowote   6 JUMLA                               51                          Hivyo ndivyo lilivyopitishwa tamko hilo na huo  ndio msimamo wa Kanisa Anglikana Tanzania kuhusu Wanawake kuamuriwa katika huduma ya Ukasisi na Ushemasi. Mheshimiwa Mwenyekiti na Wajumbe, Halmashauri ya Dayosisi yetu katika kikao chake kilichofanyika Morogoro tarehe 20 Julai 2000 ilipokea hilo tamko la Sinodi ya Jimbo na ikaazimia kama ifuatavyo: Nanukuu “ Kwa kuwa hoja hiyo ilishawekewa msimamo na Sinodi ya Jimbo; Dayosisi ya Morogoro tutabaki na uamzi huo hadi hapo jambo hilo litakapoonekana kwamba ,linahitaji  kujadiliwa tena .” KUZINGATIA UTARATIBU ULIOWEKWA NA NYUMBA YA MAASKOFU Nyumba ya Maaskofu ili kulinda Umoja katika Kanisa na kuhifadhi utulivu, ilitoa mwongozo wa utaratibu utakaofuatwa iwapo dayosisi inaweka wanawake kuwa wachungaji; a)  Wanawake wanaoamuriwa watumike katika Parishi au pale huduma yao inapopokelewa na kukubaliwa. b)  Waumini  ambao bado hawaikubali huduma ya uchungaji ya wanawake wasilazimishwe c)  Wachungaji wanawake  watakaoamuriwa watakuwa wa dayosisi inayowakubali na madayosisi yasiyo wakubali hayatalazimika kuwakubali.