Перейти к содержимому

Salama Na RUBY SE6 EP18 |KIDANI PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

YahStoneTown

0:00 / 0:00

Salama Na RUBY SE6 EP18 |KIDANI PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

68 409 просмотров · 4 года назад
YahStoneTown
412 тыс. подписчиков
68 409 просмотров · 4 года назад
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 KIDANI Maisha yanakua na muonekano mwengine kwa yule ambaye anakua anayaangalia kwa mbali kwasababu ki ukweli kabisa anakua anaona vitu si kwa uhalisia ule ambao ni wa kweli. Suala la Ruby kutokua na heshima au kukitumia kipaji chake vile itakiwavyo limekua likiongelewa mara nyingi na watu wa kawaida ambao ni mashabiki wa muziki wake lakini pia na ‘wadau’ mbalimbali ambao kwa namna moja ama nyengine wamekua wakimskiliza na kuupiga mziki wake au hata kuuza sehemu mbali mbali hapa duniani, wao wanaamini kabisa na wengine hata hawafichi kwamba Binti huyu Mwenye kipaji kikubwa kama tu angekua na HESHIMA na AKASKILIZA aambiwacho basi ‘angekua mbali sana’. Je, tulishawahi kufikiria kwani Ruby mwenyewe anasemaje kuhusiana na ‘shutuma’ hizi nyingi ambazo huja upande wake? Maneno kama haya ambayo amekua akiyaskia mara kwa mara? Yanafanya ajiskiaje hasa? Na ni kweli iko hivyo? Ni kweli yeye ni MJEURI na HASKILIZI watu? Ni kweli baadhi ya tabia zake ndo ZINAZO MCHELEWESHA? Binti huyu siwezi kusema ni Rafiki yangu kabla ya maongezi haya, mimi na yeye tulishawahi kuongea kidogo miaka miwili hivi iliyopita na yalikua maongezi ya kazi ambayo alikuja na ikaenda tu vizuri, miaka miwili na ushee baadae ndo nikamtafuta tena ili tuweze kuyajenga kwenye meza yetu ya kipindi hiki. Na wala haikua kazi ya kumuingiza tembo bandani, tulifanya tu makubaliano ya kawaida kabisa na siku ya kazi alitokea tu vizuri. Tukaongea, akayajibu maswali yangu ambayo yalikua mengi na kwa ufasaha tu. Kwangu alikua charming, easy going na tulielewana tu poa. Tuliongelea kuhusu makuzi yake na familia yake, mahusiano yake na THT ambayo miaka ya nyuma wakati wa uhai wa Ruge Mutahaba kulikua na maneno mengi kuhusu mahusiano yao wawili hawa pamoja na mabinti wengine ambao nao walikua kwenye kituo hicho miaka hiyo. Tuongelea kipaji chake, Mungu alivyombariki na mtoto hivi karibuni, suala la yeye kuwa mapenzini, kuachwa na jinsi ambavyo anakabiliana na maneno mengi ambayo yamekua yakisemwa juu yake. Huwa anajiskiaje? Anapambana vipi? Maongezi yalikua ya kugusa ila binafsi pia session hii ilikua ya mitihani mingi. Hii siku ndo nilipokea taarifa ya kifo cha Rafiki na Dada yangu Sylvia Mambiu Shekilango ambaye alikua hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha wagonjwa wa moyo kule akipambania uhai wake baada ya operesheni kubwa ya moyo. Ilikua ngumu kwangu ila kazi ilibidi iendelee. Namshkuru Mungu kwa maisha yake na urafiki wetu. Mungu Amsamehe Makosa Yake Na Amrehemu. Kipindi hiki kiko dedicated Kwake. Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬ ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬ GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible & Msam...   Follow: Twitter:   / yahstonetown   Instagram:   / yahstonetown   Facebook:   / yahstonetown   Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz