Перейти к содержимому

MHE OTHMAN MASOUD: TOFAUTI ZA VYAMA ZISITUGAWANYE, TUSHIKAMANE KUJENGA ZANZIBAR”

Tifu Tv

0:00 / 0:00

MHE OTHMAN MASOUD: TOFAUTI ZA VYAMA ZISITUGAWANYE, TUSHIKAMANE KUJENGA ZANZIBAR”

755 просмотров · 12 часов назад
Tifu Tv
44,6 тыс. подписчиков
755 просмотров · 12 часов назад
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT, wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba pamoja na kuwepo tofauti za vyama kisiasa, lakini ni muhimu wananchi wote kuendeleza mshikamano ili kuijenga nchi yao na kwamba vyama vya siasa visiwagawe kwa kuwa ni hiari ya mtu mwenyewe kuchagua akitakacho. Mhe. Othman ambaye pia ni makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo alipozungunza na wanabarza ya Wazee iliyopo Kijuki wilaya ya Wete Jimbo la Pandani Mkoa wa kaskazini Pemba baada ya kuizindua rasmi baraza hiyo ikiwa ni jitihada za kuimarisha chama hicho. Amefahamisha kwamba vyama vinaweza kutazamwa na kuchukuliwa kama uraibu wakati mwengine kwa watu wengine na baadhi kutumia mazoea , lakini wananchi wote wanawajibika kuendeleza mshikano na umoja kwa kueleta maendeleo ya nchi yao. Kwa upande mwengine Mhe. Othman amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kihakikisha wanafanya juhudi kubwa za kuimarisha chama chao kwa kuwa ndio chombo muhimu kinachotumika katika kufikia lengo la kuleta mageuzi na maendeleo ya taifa lao. Amesema kwamba ni lazima wanachama wajitahidi kuimarisha barza za chama hicho ili kuwa madhubuti na kufanya kazi za chama wanazoelekezwa kwa ufanisi mkubwa kuwa barza ndio kituo cha mwanzo muhimu kuelekea matawi, Jimbo Mkoa na taifa lakini unapokuwa na chama dhaifu na serikali pia itakuwa dhaifu. Hata hivyo Mhe. Othman amewaomba wananchi wa Zanzibar kuendelea kuwaamini viongozi wao na kwamba lengo la kuungana katika serikali ya umoja wa kitaifa ni kuhakikisha kwa pamoja wanasimamia utekelezaji wa maridhiano yaliyofikiwa kwa kuwa ramani ya kazi hiyo tayari imeandaliwa. Amewashukuru wananchi wote wa Zanzibar na hasa wafuasi wa chama hicho kwa kufahamu sababu za viongozi hao kuchelewa kujiunga na serikali ya Umoja wa kitaifa lakini lengo kubwa ni kuwepo mashirikiano katika kutekeleza yaliyokubalika kwenye maridhiano. Hata hiovyo,amesema kwamba kulingana na historia ya vyama vingi hapa Zanzibar, wazanzibar waleowengi kwa muda mrefu sasa wanatamani na wanahitaji kupata maegeuzi ili kukidhi kiu ya kuharakisha mendeleo ya kiuchumi na kijamii ndani ya nchi yao. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ACT wazalendo upande Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, amesema kwamba maalim Seif kama kiongozi wa kisiasa alikubalika kwenye visiwa vya Zanzibar na nje ya Zanzibar baada ya juhudi kubwa ya kisiasa na kupewa heshima kubwa liliyoanzia kijijini kwao Mtambwe na kuwaomba wanamasipa nao kufanya kama walivyofanya wana wa Mtambwe. Naye Mwenyekiti wa Barza hiyo ya wazee Masipa Maalim Bakari Sharif, amewashukuru wananchi pamoja na mwenyekiti wa taifa kwa kwa jitihada na maono aliyonayo katika kusaidia juhudi za pamoja za kuimarisha chama kwa nia kufikia malengo ya chama hicho kuleta mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kuchapuza maendeleo. Aidha amewataka vijana wa Zanzibar kujitahidi katika kujiandaa kuwa mbadala wa viongozi mbali mbali kwa kuwa waliotangulia kujengewa uwezo wa kumudu kushika nafasi mbali mbali za kusimamia mageuzi kupitia vyama vyao kama alivyofanya marehemu Malim seif kuwaandaa viongozi ambao kazi za chama licha ya kutangulia ,mbele ya haki lakini zinasimamiwa na kuendelea vyema kama inavyonekana hapa Zanzibar. Mhe. Othman yupo kisiwani Pemba kwa ziara ya siku mbili ambapo jana alihotubia mkutano wa hadhara uliokuwa na madhumuni ya yeye kupongezwa kwa kuteuliwa na kula kiapo cha umakamu wa Kwanza wa rais kufuatia kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa yaliyosainiwa Julai tisa mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine utekelezaji wake pia ni ushiriki rasmi wa ACT katika serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar.