LIVE:WAKATI LISSU AKISUBIRI HUKUMU YA UHAINI, BUNGE LA ULAYA LAMUINGIZA TUZO YA SAKHAROV
HARAKATI TV
0:00 / 0:00
LIVE:WAKATI LISSU AKISUBIRI HUKUMU YA UHAINI, BUNGE LA ULAYA LAMUINGIZA TUZO YA SAKHAROV
54 143 просмотра · Трансляция закончилась 6 ч назад
HARAKATI TV
100 тыс. подписчиков
54 143 просмотра · Трансляция закончилась 6 ч назад
LIVE:WAKATI LISSU AKISUBIRI HUKUMU YA UHAINI, BUNGE LA ULAYA LAMUINGIZA TUZO YA SAKHAROV
Wakati Tanzania ikisubiri hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, jina lake limewasilishwa rasmi katika kinyang’anyiro cha Tuzo ya Sakharov ya Uhuru wa Mawazo ya Bunge la Ulaya.
Katika video hii tunachambua kwa kina hatua hii mpya, nani amewasilisha jina la Lissu, sababu zilizotolewa na makundi ya Bunge la Ulaya yanayomuunga mkono, pamoja na historia yake ya kisiasa inayohusishwa na uteuzi huo.
ECR imetaja miongoni mwa sababu za kumuunga mkono Lissu ni msimamo wake kuhusu uchaguzi huru na wa haki, utawala wa kikatiba, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria. Kundi hilo pia limekumbusha shambulio la mwaka 2017 ambalo Lissu alipigwa risasi mara kadhaa na kunusurika.
Wakati huo huo, EPP pia limetangaza kumuunga mkono Lissu, likisema uteuzi huo unatuma ujumbe kuhusu demokrasia na utawala wa sheria nchini Tanzania.
Lakini je, Lissu tayari ameshinda Tuzo ya Sakharov?
Hapana. Uteuzi huu ni hatua ya mwanzo katika mchakato ambao bado unaendelea. Majina matatu yanatarajiwa kuchaguliwa kwa hatua ya mwisho Oktoba 19, kabla ya mshindi kuchaguliwa Oktoba 22. Sherehe ya utoaji wa tuzo imepangwa kufanyika Desemba mjini Strasbourg.
Kwa upande mwingine, Tanzania inaendelea kusubiri hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Lissu. Baada ya pande zote kukamilisha hoja zao za mwisho Septemba 29, Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga Novemba 6, 2026 kuwa siku ya kusoma hukumu.
Hivyo, Oktoba hii inamkuta Tundu Lissu katikati ya michakato miwili muhimu: mchakato wa kesi ya uhaini nchini Tanzania na mchakato wa kuwania Tuzo ya Sakharov barani Ulaya.
Tazama video hadi mwisho kwa uchambuzi wa kina wa kinachoendelea, hatua zinazofuata na maana ya jina la Lissu kuingia rasmi kwenye kinyang’anyiro hiki.
#TunduLissu #KesiYaUhaini #Chadema #Jamhuri #MahakamaKuu #Tanzania #Lissu #SiasaTanzania #HabariTanzania #Uchambuzi