Huu Hapa Uchambuzi wa Kesi Dhidi ya Serikali Kuhusiana na Matukio ya Okt. 29
The Chanzo
0:00 / 0:00
Huu Hapa Uchambuzi wa Kesi Dhidi ya Serikali Kuhusiana na Matukio ya Okt. 29
11 185 просмотров · 9 мес. назад
The Chanzo
261 тыс. подписчиков
11 185 просмотров · 9 мес. назад
The Chanzo imezungumza na Wakili Jebra Kambole kuhusiana na kesi mbili zilizofunguliwa dhidi ya Serikali Mahakama Kuu kufahamu msingi wa kesi hizo, ikiwemo matamko waliozifungua wanataka Mahakama itamke.
Kesi hizo ni ile inayohusiana na amri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Camillus Wambura ya Oktoba 29, 2025, ya kutaka watu wawe majumbani mwao kuanzia saa 12 jioni, na ile inayohusu Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuchunguza kile kilichotokea Oktoba 29 ambapo mamia ya watu wanahofiwa kuuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kambole, ambaye ni moja wapo wa mawakili wanaowakilisha waleta maombi kwenye kesi hizo, anasema kwamba mambo yote hayo mawili yamefanywa kwa kukiuka misingi ya sheria na Katiba za nchi, na wateja wake wanaitaka Mahakama ikubaliane nao kwenye ombi hilo, na kutoa amri zingine zilizoombwa.
You can follow us via;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Or visit our website: https://www.thechanzo.com
Do you have news? contact us via Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.