Перейти к содержимому

RC SAGINI: HAKUNA KUMKINGIA KIFUA DEREVA WA BAJAJI AU BODABODA ANAYEVUNJA SHERIA!

The Green Voice TV

0:00 / 0:00

RC SAGINI: HAKUNA KUMKINGIA KIFUA DEREVA WA BAJAJI AU BODABODA ANAYEVUNJA SHERIA!

1 741 просмотр · 9 дней назад
The Green Voice TV
2,84 тыс. подписчиков
1 741 просмотр · 9 дней назад
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Jumanne Sagini, amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Benjamini Kuzaga, kuwachukulia hatua za kisheria madereva wa bajaji, bodaboda na daladala wanaokiuka sheria za barabarani kwa makusudi. Sagini amesema tabia ya baadhi ya madereva wa bajaji na pikipiki kutofuata sheria imekuwa kero kwa wananchi wa Jiji la Mbeya. Ameeleza kuwa baadhi ya madereva hao hujivunia kuwa vyombo vyao vinamilikiwa na viongozi wa serikali na watu wenye ushawishi, jambo ambalo halipaswi kuwakinga dhidi ya sheria. Aidha, Sagini amesisitiza kuwa hatamkingia kifua dereva yeyote atakayekamatwa kwa kuvunja sheria za barabarani, hata kama atapigiwa simu na kiongozi anayemiliki chombo hicho. Ameyasema hayo leo alipokutana na wafanyabiashara, madereva, taasisi mbalimbali pamoja na watendaji wa kata na mitaa, akitaka changamoto hizo zishughulikiwe kwa mujibu wa sheria.