TAHARUKI! WAKULIMA VS WAFUGAJI, WATATU WAUAWA MMOJA AZAMISHWA KWENYE TOPE, 25 MBARONI
ITV Tanzania
0:00 / 0:00
TAHARUKI! WAKULIMA VS WAFUGAJI, WATATU WAUAWA MMOJA AZAMISHWA KWENYE TOPE, 25 MBARONI
160 просмотров · 1 час назад
ITV Tanzania
1,37 млн подписчиков
160 просмотров · 1 час назад
#HABARI: Watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mfululizo wa matukio yanayodaiwa kuchochewa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limewakamata watu 25 wanaodaiwa kuhusika na mauaji na vurugu hizo.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, baada ya kufika katika maeneo yaliyoathiriwa na kujionea uharibifu wa mali uliotokana na vurugu hizo, ikiwemo kuchomwa kwa ofisi za Serikali na kuharibiwa kwa gari la Polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda Chilya, kati ya watuhumiwa 25 waliokamatwa, wanane wanahusishwa na matukio ya mauaji huku 17 wakihusishwa na vurugu, ambapo wafugaji ni 10 na wakulima 15 ambapo ameongeza kuwa operesheni na upelelezi vinaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wengine.
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ;
Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3
Twitter : https://bit.ly/2XG7aii
Instagram : https://bit.ly/34KItmg