Перейти к содержимому

TAFAKARI YA SIKU JUMATATU YA JUMA LA 6 MWAKA C 18.02.2019

KANISA KATOLIKI TANZANIA TEC

0:00 / 0:00

TAFAKARI YA SIKU JUMATATU YA JUMA LA 6 MWAKA C 18.02.2019

1 336 просмотров · 7 лет назад
KANISA KATOLIKI TANZANIA TEC
136 тыс. подписчиков
1 336 просмотров · 7 лет назад
TAFAKARI YA NENO LA MUNGU, JUMATATU TAREHE 18/02/2019 Somo: Marko 8:11-13 Utangulizi Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, karibuni katika tafakari ya neno la Mungu leo jumatatu ya juma la 6 la mwaka tarehe 18/2/ 2019. Tusikilize kwanza neno la Mungu. Fundisho kuu katika neno la Mungu tulilolisikia hivi punde ni Ishara na Miujiza. Katika somo la leo, tumesikia habari za mafarisayo wakitaka ishara kutoka kwa Yesu. wanaomba ishara hiyo kwa lengo la kumjaribu. Pia, muda wanaoomba ishara, tayari Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa ameshafanya miujiza mingi kama vile kuwaponya wagonjwa mbalimbali (Rejea Injili ya Mathayo 8:5-13), kuwalisha maelfu ya watu kwa mikate na samaki wachache (Luka 8:1-8) na kuwaponya vipofu (Rejea Injili ya Mathayo 7:51-52). Kwa hakika kabisa, miujiza yote ambayo Yesu alifanya, mafarisayo waliiona kwa macho au kuisikia kupitia masimulizi ya walioishuhudia. Kumbe walikuwa wanajua nguvu na uwezo wa Bwana wetu Yesu Kristo. Miujiza hiyo ilikuwa ishara tosha kwa wao kusadiki kuwa kweli alikuwa ametoka kwa Mungu nae ndiye mwana wa Mungu kama alivyokuwa akihubiri. Leo mafarisayo wanapoomba ishara, hawaombi tu uponyaji wa wagonjwa au kufanya mambo mengine yenye kupita fahamu za kibinadamu, bali wanataka Yesu atoe ishara ya kimiuijiza iliyo wazi na ya moja kwa moja kutoka mbinguni ili iwahakikishie kuwa kweli ametoka kwa Mungu. Yesu anakataa kutoa ishara hiyo akijua wazi kuwa kama wangekuwa ni watu wa kuamni, wangekuwa tayari wameamini kupitia kazi zake. Kukataa kwake kutoa ishara, kupanda chomboni na kuondoka, kunaonesha wazi kabisa kuwa Yesu hakufurahishwa na tabia ya mafarisayo. Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, tunaposoma maandiko matakatifu, hasa katika injili, mara nyingi tunasoma habari za Yesu akiwakemea kwa nguvu Mafarisayo huku akiwapa OLE nyingi endapo wataendelea kuwa watu wa tabia na mienendo ileile waliyoizoea kama unafiki na majivuno, (Rejea Mt. 23:13-24, Lk 18:9-14). Kwa kuwa mambo mengi waliyoyafanya Mafarisayo yalikemewa na Bwana wetu Yesu Kristo, tutambue kuwa mafarisayo sio mfano mzuri wa kuigwa na sisi Wakristo. Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, inawezekana kuwa hata sisi katika maisha yetu, huenda tunaushiriki ufarisayo kwa namna zetu za kufikiria, kusema na kutenda. Somo la leo linatutaka tusiwe kama wafarisayo, yaani watu wa kudai ishara ili tuamini. kudai ishara ni dalili ya mashaka, na hivyo Kristo hafurahishwi na yeyote mwenye kumtilia mashaka. Sisi kama ilivyokouwa kwa wafarisayo, tayari tunazo ishara nyingi zenye kutupa nguvu ya kumuamini na kumfuasa Kristo. Kati ya ishara hizo, iliyo kubwa Zaidi ni ile ya fumbo la Pasaka, yaani mateso kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambayo Yesu aliwajibu kwa mafumbo wale waandishi na mafarisayo kuwa hawatapewa ishara nyingine zaidi ya ile ya Nabii Yona (Rejea Mt. 12:38-40). Katika maisha yetu ya sasa mafarisayo hawana tofauti na makundi mbalimbali ya watu yanayoibuka sana siku hizi. Makundi hayo yanasisitiza sana juu ya miujiza kama uponyaji wa magonjwa kwa njia ya maombi au kutoa pepo kuwa ndio ishara ya uwepo wa Mungu wa kweli. Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, sisi kama wakristo tukiongozwa na neno la Mungu la siku hii ya leo, kamwe tusiyumbishwe na upepo wa kifarisayo, badala yake tuipokee, tuamini na kuiishi ishara kubwa pekee aliyoisema Kristo mwenyewe, yaani ile ya Nabii Yona. Bila ishara hiyo ya Nabii Yona, hakuna wokovu. Tusitafute ishara zaidi, kwani kwa kufanya hivyo Bwana wetu yesu Kristo ataugua rohoni mwake na kwa maana hiyo, sisi pia tutahesabika miongoni mwa mafarisayo wa nyakati hizi ambao Yesu aliwapa “Ole” nyingi kama watakuwa watu wa kushikilia yale yanayowapendeza wao na kuacha anayowaagiza. Mungu mwenyezi atusaidie tusimame imara katika imani yetu, ili ishara na miujiza isiwe kitu cha lazima katika imani yetu kwa Kristo. Tumsifu Yesu Kristo! Tafakari hii imetolewa na mimi, Frt. Emmanuel Simanwe, wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mwaka wa pili wa Theolojia, Seminari Kuu ya Kipalapala – Tabora.