Перейти к содержимому

AICT Chang’ombe Choir - Saa ya Mwisho (Official Music Video)

AIC Chang'ombe Choir (CVC)

0:00 / 0:00

AICT Chang’ombe Choir - Saa ya Mwisho (Official Music Video)

377 710 просмотров · 3 года назад
AIC Chang'ombe Choir (CVC)
184 тыс. подписчиков
377 710 просмотров · 3 года назад
Shalom Shalom Mpendwa Katika Bwana! Imekuwa baraka sana kukuletea wimbo huu wa saa ya mwisho ikiwa kama zawadi yetu ya Pasaka kwako. LUKA 23:32-43 Wimbo huu unaeleza namna gani tunatakiwa kuutumia muda tulionao vizuri, mfano wa wanyang’anyi wawili walipokuwa pamoja na YESU msalabani, mmoja aliamua kuitumia saa yake ya mwisho vizuri, akasema ‘’Ee YESU! unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako” ingawa alikuwa mtenda dhambi lakini YESU alimwambia Leo hii utakua pamoja nami peponi. Haijalishi umefanya maovu kiasi gani, umepitia magumu mangapi bado nyumbani mwa BWANA una nafasi unachotakiwa ni kutubu, kuacha njia mbaya na kumgeukia BWANA ili ukaurithi ufalme wake wa milele. #Saayamwisho #pasaka #choir SONG LYRICS; Kiitikio : Saa ya mwisho kumbuka inakuja Kumbuka..saa ya mwisho karibu inakuja Iyo..oooh x2 Beti 1: Wanyang’anyi wawili msalabani wakiwa naye YESU Wanangojea kifo msalabani wakingojea kifo Wenye dhambi wawili msalabani wakiwa naye YESU Saa yao ya mwisho msalabani wakingojea kifo. Wenye dhambi wawili msalabani wakiwa naye YESU Saa yao ya mwisho msalabani wakingojea kifo. Solo 1 : Iye iye iye iye iye Baba ooh : Iye iye iye iye iye ooh Wa kwanza alianza kumwambia Bwana YESU Kwa kejeli alianza kumwambia Bwana YESU Ulijifanya MUNGU..mbona unateseka Kama wewe ni MUNGU ebu jiponye sasa Ulijifanya MUNGU, mbona unateseka Kama wewe ni MUNGU ebu jiponye sasa tuponye na sisi Yesu hakujibu (Yesu hakujibu) x2 Kiitikio : Saa ya mwisho kumbuka inakuja Kumbuka..saa ya mwisho karibu inakuja Iyo..oooh X2 Solo 2 : Wa pili alianza kumwambia Bwana YESU Kwa adabu alianza kumwambia Bwana YESU Mimi ni mwenye dhambi Naomba msamaha Unikumbuke Baba unakokwenda Baba Nimetenda maovu naomba msamaha Unikumbuke Baba unakokwenda Baba..(Aaaah) Unikumbuke Baba unakokwenda Baba..(Aaaah) Solo : Yesu alijibu Wote: (Yesu alijibu) x2 Leo hii utakua nami peponi Leo hii utakua nami mbinguni Leo hii.. Kiitikio : Saa ya mwisho kumbuka inakuja Kumbuka..saa ya mwisho karibu inakuja Iyo..oooh x2 SONG CREDITS TO; Song Writer - Papaa Clement Buhembo Video Director - Elidadi Videographer - Amigo Johnson Lights - Sengati Audio - CVC Media Tufuatilie kupitia Instagram   / cvcchoirtz_official   Facebook   / cvc-choir   ©2023 AICT Chang'ombe Choir | All Rights Reserved.Channel Administered by Huru Digital Instagram:   / hurudigital