WATOTO WENYE CHANGAMOTO WATAKIWA KUPENDWA NA KULINDWA
CTV NEWS TANZANIA
0:00 / 0:00
WATOTO WENYE CHANGAMOTO WATAKIWA KUPENDWA NA KULINDWA
63 просмотра · 3 нед. назад
CTV NEWS TANZANIA
167 подписчиков
63 просмотра · 3 нед. назад
Serikali imesema itaendelea kutoa sapoti kwa watoto wenye changamoto mbalimbali, wakiwemo wanaotumia mfumo maalum wa kujisaidia haja kubwa na haja ndogo pamoja na changamoto za mfumo wa uzazi.
Akizungumza katika maadhimisho yaliyofanyika Kidutani, Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu, Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga, amesema jamii inapaswa kuwapa watoto hao upendo, malezi na ulinzi, na kutowaona kama laana au matokeo ya kurogwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Healthy Children Organization, Mtumwa Sulaiman Hamza, amesema maadhimisho hayo yamelenga kuelimisha jamii kuhusu kuwalinda na kuwahudumia watoto hao, kwa kauli mbiu “Upendo ni dawa, faraja ni tiba, matumaini ni uhai.”
Wazazi wa watoto hao wamesema, licha ya mitazamo hasi kutoka kwa jamii, wanaendelea kuwapenda na kuwalea, huku wakiiomba serikali, taasisi na jamii kuzisaidia familia hizo ili watoto wapate matibabu, elimu na fursa sawa za kutimiza ndoto zao.