Nchimbi Anaondoka — Je, Mfumo Unabadilika? | Elimuraia
Elimuraia
0:00 / 0:00
Nchimbi Anaondoka — Je, Mfumo Unabadilika? | Elimuraia
17 222 просмотра · 7 дней назад
Elimuraia
403 подписчика
17 222 просмотра · 7 дней назад
Emmanuel Nchimbi amejiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Lakini hapa Elimuraia, swali letu si tu nani anaondoka na nani anakuja. Swali kubwa zaidi ni: Je, mfumo wenyewe unabadilika?
Katika kipindi hiki tunatumia tukio la kuondoka kwa Nchimbi kama nafasi ya kuchunguza dhana muhimu katika sayansi ya siasa: uhalali (legitimacy), uhalalishaji (legitimation), taasisi za kisiasa, na tofauti kati ya mabadiliko ya viongozi na mabadiliko ya mfumo wa madaraka.
Tunarejea pia uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, mjadala wa Katiba Mpya, utawala wa John Pombe Magufuli, mwanzo wa utawala wa Samia Suluhu Hassan, na falsafa ya 4Rs.
Hoja kuu ni rahisi:
Katika siasa, usivutiwe sana na majina. Angalia taasisi. Angalia kanuni. Angalia mfumo wa madaraka.
⚠️ TAARIFA MPYA:
Video hii ilirekodiwa kabla ya matukio ya hivi karibuni kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais. Baada ya kurekodiwa, CCM ilitangaza kumfukuza Emmanuel Nchimbi katika chama na kumpitisha Deogratius Ndejembi kama anayependekezwa kuchukua nafasi hiyo.
Leo, tarehe 29 Agosti 2026, Deogratius Ndejembi ameapishwa rasmi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Bunge kuidhinisha uteuzi wake kwa kura 324 bila kura ya kupinga.
Hata hivyo, hatua hizi hazibadili swali kuu la video hii: Je, kubadilika kwa mtu mwenye madaraka kunamaanisha kwamba mfumo wenyewe umebadilika?
Vyanzo na marejeo
David Beetham — The Legitimation of Power
Kitabu hiki ndicho msingi wa mjadala wetu kuhusu uhalali na mchakato wa kujenga uhalali.
African Union Election Observation Mission — Tanzania General Elections, 2025
Waangalizi wa Umoja wa Afrika walihitimisha kuwa uchaguzi wa 2025 haukukidhi kanuni za AU na viwango vingine vya kimataifa vya uchaguzi wa kidemokrasia, na wakataka mageuzi ya haraka ya kikatiba na kisiasa.
Taarifa ya Umoja wa Afrika kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025
[https://www.au.int/en/pressreleases/2...].
Reuters — Emmanuel Nchimbi resigns as Tanzania's Vice President
Reuters iliripoti kujiuzulu kwa Nchimbi na pia mjadala uliotangulia kuhusu mageuzi ya Katiba [https://www.reuters.com/world/africa/...].
Associated Press — Tanzania political developments following Nchimbi's resignation [https://apnews.com/article/tanzania-v...].
AP imeripoti kuhusu kujiuzulu kwa Nchimbi, kufukuzwa kwake CCM na uteuzi wa Ndejembi [https://apnews.com/article/tanzania-v...].
The Citizen — CCM expels Nchimbi, endorses Ndejembi
Taarifa kuhusu uamuzi wa CCM na hatua zinazofuata za kikatiba [https://www.thecitizen.co.tz/tanzania...].
The Citizen — Tanzania swears in new Vice President Ndejembi
[https://www.thecitizen.co.tz/tanzania...]
The Citizen — Nchimbi ceased to be Vice President on August 26 after losing CCM membership, Attorney General says
[https://www.thecitizen.co.tz/tanzania...]
Vyanzo vingine vilivyotumika katika maandalizi ya kipindi ni pamoja na BBC News Swahili, Mwananchi, ITV Tanzania, Star TV, AP News na The Citizen.
Elimuraia hailengi kukuambia uamini nini. Tunachukua dhana muhimu za sayansi ya siasa, tunazifafanua kwa Kiswahili rahisi, na kukupa msingi wa kujenga maoni yako mwenyewe.
Kabla ya kuwa na maoni, lazima kwanza tuelewe dhana.
Kujua ni kuchagua.
#Elimuraia #Tanzania #Nchimbi #KatibaMpya #Uhalali #SiasaTanzania #SamiaSuluhuHassan #Ndejembi #Demokrasia #SayansiYaSiasa