Перейти к содержимому

TANZIA: MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA MUME WA RAIS SAMIA - KIZIMKAZI

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

TANZIA: MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA MUME WA RAIS SAMIA - KIZIMKAZI

32 526 просмотров · 17 часов назад
ASAM Online TV
21,5 тыс. подписчиков
32 526 просмотров · 17 часов назад
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameongoza maelfu ya waombolezaji katika kuaga mwili wa marehemu Hafidh Ameir Hassan, ambaye alikuwa mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Marehemu Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia majira ya saa mbili asubuhi ya leo, Septemba 7, 2026, wakati alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na ugonjwa wa moyo. Marehemu anakumbukwa pia kwa kuwa mtaalamu mstaafu wa sekta ya kilimo na mifugo Zanzibar, huku akielezwa kuwa alikuwa mtu mwenye utulivu na aliyekuwa akimuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake. Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wameendelea kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, wakieleza masikitiko yao na kumkumbuka kama mume na mzazi mwenye busara. Mwili wa marehemu Hafidh Ameir Hassan umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele leo majira ya saa kumi jioni huko Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja. Asam Online TV inaungana na familia, ndugu, jamaa, viongozi na wananchi katika kipindi hiki cha majonzi, na kuwaombea wafiwa subira na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina. #Tanzia #HafidhAmeirHassan #HafidhAmeir #SamiaSuluhuHassan #Rambirambi #Kizimkazi #Zanzibar #Tanzania #AsamOnlineTV #Msiba #TanzaniaNews #ZanzibarNews #BreakingNews #NewsUpdate #Trending #TikTokTanzania #InstagramTanzania #Viral