Перейти к содержимому

TUSOME BIBLIA KILA SIKU : MWANZO SURA YA NNE

HolyDigitalTZ

0:00 / 0:00

TUSOME BIBLIA KILA SIKU : MWANZO SURA YA NNE

1 345 просмотров · 6 л. назад
HolyDigitalTZ
18 тыс. подписчиков
1 345 просмотров · 6 л. назад
EITVMEDIA    • TUSOME  BIBLIA KILA SIKU : MWANZO SURA YA NNE   MWANZO SURA YA 4 Mwanzo:4.1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Mwanzo:4.2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Mwanzo:4.3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Mwanzo:4.4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; Mwanzo:4.5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Mwanzo:4.6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Mwanzo:4.7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Mwanzo:4.8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Mwanzo:4.9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Mwanzo:4.10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Mwanzo:4.11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; Mwanzo:4.12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Mwanzo:4.13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Mwanzo:4.14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. Mwanzo:4.15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. Mwanzo:4.16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. Mwanzo:4.17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe. Mwanzo:4.18 Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki. Mwanzo:4.19 Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. Mwanzo:4.20 Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. Mwanzo:4.21 Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. Mwanzo:4.22 Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama. Mwanzo:4.23 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua; Mwanzo:4.24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba. Mwanzo:4.25 Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. Mwanzo:4.26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana.