KASEKENYA : MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUENDANA NA TEKNOLOJIA MPYA ZA MAGARI
Wizara ya Ujenzi
0:00 / 0:00
KASEKENYA : MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUENDANA NA TEKNOLOJIA MPYA ZA MAGARI
145 просмотров · 9 дней назад
Wizara ya Ujenzi
9,25 тыс. подписчиков
145 просмотров · 9 дней назад
Serikali imehimiza mafunzo endelevu kwa madereva wa Serikali ili kuwawezesha kuendana na matumizi ya magari ya kisasa yenye teknolojia mpya, ambayo yameleta mabadiliko makubwa katika mifumo ya uendeshaji na matengenezo ya magari nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, Septemba 16, 2026, wakati akifungua Kongamano la Tano la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST).
Mhandisi Kasekenya amezitaka Taasisi za Umma kutenga bajeti kwa ajili ya mafunzo ya mara kwa mara kwa madereva, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa madereva kuhusu matumizi sahihi ya magari mapya, kupunguza uharibifu unaoweza kuepukika, kuongeza usalama barabarani na kulinda thamani ya mali za Serikali.