WAT SACCOS YATAKA NIDHAMU YA MAREJESHO YA FEDHA, ELIMU YA FEDHA YASISITIZWA..
Global TV Ripota
0:00 / 0:00
WAT SACCOS YATAKA NIDHAMU YA MAREJESHO YA FEDHA, ELIMU YA FEDHA YASISITIZWA..
52 просмотра · 4 дня назад
Global TV Ripota
20,7 тыс. подписчиков
52 просмотра · 4 дня назад
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dar Es salaam amevitaka vyama vya ushirika vya akiba na mikopo kuzingatia weledi na uadilifu katika kuendesha vyama hivyo ambavyo vimekuwa msaada katika kuwezesha mikopo na mitaji kwa wafanyabiashara na wa wajasiriamali nchini
Akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha WAT SACCOS, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dar es Salaam, Anjela Nalimi, amesisitiza kuwa uadilifu na weledi vinapaswa kuwa mwongozo katika kuendesha vyama hivyo ili kuviwezesha kuendelea kuwa imara, huku serikali ikivitazama kama njia ya kuwawezesha wananchi kupata mitaji.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa WAT SACCOS, Bazir Kimario, amesema chama hicho kimepanga kutoa jumla ya mikopo 352 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6 kwa wanachama wake, ikiwa ni ongezeko la asilimia 147 ikilinganishwa na mikopo 190 iliyotolewa mwaka uliopita.
Naye Afisa Mtendaji wa WAT SACCOS, Marry Sanga, amesema mafanikio ya chama hicho yamechangiwa na utendaji bora wa uongozi, hali iliyowezesha kuongezeka kwa idadi ya wanachama na wanufaika hadi kufikia 23,000.
Kwa upande wake, Mjumbe wa WAT SACCOS, Prosper Ernest, amegusia changamoto ya baadhi ya wanachama kuchelewa kurejesha mikopo, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya mikopo na fedha kwa vijana ili kuwawezesha kuelewa madhumuni ya kukopa na kulinda uendelevu wa vyama vya akiba na mikopo.
#globaltvonline #globaltvripota
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx