Chamwino Mguu Sawa Kuikabili El Niño
Chamwino Dc
0:00 / 0:00
Chamwino Mguu Sawa Kuikabili El Niño
2 просмотра · 1 день назад
Chamwino Dc
98 подписчиков
2 просмотра · 1 день назад
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa tahadhari kwa wananchi wa Kata ya Manchali na Wilaya ya Chamwino dhidi ya mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha kwa wingi kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu.
Ametoa tahadhari hiyo jana tarehe 22, 2026 baada ya kushiriki zoezi la usafi pamoja na wananchi na kukagua daraja na korongo katika eneo la Chalinze Nyama.
RC Senyamule amezitaka kamati zote za maafa ngazi ya vijiji na kata kuhakikisha wanachukua tahadhari zote dhidi ya El Niño ikiwemo kuandaa mikakati ya namna ya kukabiliana na mvua hizo pamoja na kuandaa maeneo maalum ya kuhudumia wananchi endapo kutatokea madhara.
Aidha, Mhe. Senyamule amewataka wataalam wote kuhakikisha kufanya kazi ya ziada kuzuia na kukabiliana na athari zote zitakazosababishwa na mvua za El Niño ili kupunguza adha kwa wananchi.