“TUJIANDAE NA KIFO…’ MUFTI ASEMA TUTENDE YANAYOMPENDEZA MUNGU
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
“TUJIANDAE NA KIFO…’ MUFTI ASEMA TUTENDE YANAYOMPENDEZA MUNGU
817 просмотров · 1 день назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
817 просмотров · 1 день назад
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewataka Waislamu kujiandaa na safari ya ahera, ambayo kila mmoja atakwenda, hivyo wanapaswa kufanya matendo mema yanayompendeza na kumridhisha Mwenyezi Mungu.
Sheikh Zubeir ameeleza hayo leo Jumamosi Septemba 26, 2026 katika hitima ya kumuombea aliyekuwa mume wa Rais Samia Suluhu Hassan, hayati Hafidh Ameir Hassan iliyoandaliwa na familia ya Ameir iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Hitima hiyo imefanyika ukumbi wa Diamond imehudhuriwa na masheikh, maaskofu, wachungaji, mawaziri, manaibu waziri na wakuu wa taasisi, viongozi 12 wa vyama vya siasa na mabalozi wa Uturuki, Comoro, UAE, Yemen, Syria na Misri.
Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbumbuku ya Mzena, Zanzibar alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Amesisiza Waislamu na Watanzania kujiandaa na safari ya kifo kwa kuhakikisha wanatenda au kufanya mambo mema na siyo yanayomchukiza Mwenyezi Mungu.