Перейти к содержимому

NIPE FAGIO YAKABIDHI KITUO CHA KUCHAKATA TAKA KWA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

Tangajiji tv

0:00 / 0:00

NIPE FAGIO YAKABIDHI KITUO CHA KUCHAKATA TAKA KWA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

7 просмотров · 2 дня назад
Tangajiji tv
226 подписчиков
7 просмотров · 2 дня назад
Taasisi ya Nipe Fagio imekabidhi rasmi Kituo cha Kuchakata Taka kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kilichopo kata ya Chumbageni, mradi ambao umeweza kutoa ajira kwa vijana 17. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Mhe. Habibu Mpa, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kati, amewataka vijana kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi, huku akimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha vijana hao wanapatiwa POS ili kuwawezesha katika ukusanyaji wa mapato. Naibu Mkurugenzi wa Nipe Fagio Nicole Kapesi amesema kituo hicho kimekusanya na kurekodi tani 37.67 za taka kati ya Julai 27 na Agosti 31, huku akiomba Halmashauri kukitunza na kukiendeleza.