JE, MBEGU ZA ASILI ZIPO HATARINI KUTOWEKA?
ASALO TV Online
0:00 / 0:00
JE, MBEGU ZA ASILI ZIPO HATARINI KUTOWEKA?
4 просмотра · 15 ч назад
ASALO TV Online
7,7 тыс. подписчиков
4 просмотра · 15 ч назад
JE, MBEGU ZA ASILI ZIPO HATARINI KUTOWEKA?
Kwa miaka mingi, wakulima Tanzania wamekuwa wakihifadhi na kutumia mbegu za asili zilizorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Hata hivyo, ongezeko la matumizi ya mbegu za kisasa limeibua mjadala kuhusu mustakabali wa mbegu hizo, huku baadhi ya wakulima wakihofia kupungua au kupotea kwa aina mbalimbali endapo hazitaendelea kuzalishwa na kuhifadhiwa.
Wakulima na wadau wa kilimo, akiwemo Geoffrey Loibagunti wa Usariva, wanaeleza umuhimu wa kuendelea kuhifadhi mbegu za asili pamoja na maarifa yanayohusiana nazo.
Taasisi na mashirika mbalimbali, ikiwemo IDP, MVIWAARUSHA, SHIWAKUTA, TABIO na ECHO, zinaendelea kushirikiana na wakulima katika kuhamasisha uhifadhi na uzalishaji wa mbegu.
Kwa upande mwingine, ASA inaendelea kuzalisha mbegu za kilimo na kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi ya mbegu bora.
Swali kubwa linabaki: Je, tunafanya vya kutosha kuhakikisha mbegu za asili na maarifa yake havipotei kwa kizazi kijacho?
Mimi ni Abel Said Lowassa – Asalo TV Online.