WAFANYABIASHARA WA KATI NA WADOGO 10,000 KUNUFAIKA NA MAFUNZO KUTOKA BENKI YA CRDB
NEWS UPDATE MEDIA
0:00 / 0:00
WAFANYABIASHARA WA KATI NA WADOGO 10,000 KUNUFAIKA NA MAFUNZO KUTOKA BENKI YA CRDB
44 просмотра · 1 месяц назад
NEWS UPDATE MEDIA
21,6 тыс. подписчиков
44 просмотра · 1 месяц назад
WAFANYABIASHARA WA KATI NA WADOGO 10,000 KUNUFAIKA NA MAFUNZO KUTOKA BENKI YA CRDB NCHI NZIMA
MTANGAZAJI:
Takribani wafanyabiashara wa kati na wadogo 10,000 nchini wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa biashara na elimu ya fedha yatakayotolewa na Benki ya CRDB kupitia programu maalum itakayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.
Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wafanyabiashara kuongeza ufanisi wa biashara zao, kuboresha usimamizi wa fedha, kutumia fursa za kidijitali pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha zinazochochea ukuaji wa biashara.
Akizungumza kuhusu mpango huo Meneja wa kanda ya ziwa wa Benki ya CRDB Denis Mwoleka wamesema benki hiyo inaendelea kuwekeza katika kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuwapatia maarifa na suluhisho za kifedha zitakazowawezesha kukuza biashara zao na kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa.
Programu hiyo inatarajiwa kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Benki ya CRDB za kuendelea kuwa mshirika wa maendeleo ya sekta binafsi na kukuza uchumi jumuishi kupitia uwezeshaji wa wafanyabiashara wa ngazi zote.