Перейти к содержимому

SIKU 10 ZA MAOMBI 2025 || SIKU YA 1 || KAENI NDANI YANGU

The Gospel Media

0:00 / 0:00

SIKU 10 ZA MAOMBI 2025 || SIKU YA 1 || KAENI NDANI YANGU

3 193 просмотра · 1 год назад
The Gospel Media
9,38 тыс. подписчиков
3 193 просмотра · 1 год назад
SIKU 10 ZA MAOMBI 2025 | BALI WEWE USALIPO SIKU YA 1 | JAN. 8 | KAENI NDANNI YANGU Fungu Elekezi: “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yohana 15:5). Kudumu Kuunganishwa—Hitaji kwa Ajili ya Kuzaa Matunda Baada ya kuhitimu niliitwa kutumika kwenye mtaa wenye makanisa madogo matatu. Ulikuwa ni wakati wa majira ya baridi. Moja ya makanisa lilikuwa na washiriki wazee. Katika kila Sabato hasa yenye tukio maalum, tulikuwa na watu takribani 40. Kwenye Sabato ya kawaida tulikuwa na watu takribani 10. Sabato moja kulikuwa na baridi sana, ilikuwa takribani nyuzi joto -30 na watu tisa walihudhuria: familia yangu ya watu wanne na wengine watano. Niliwaza, je, nihubiri? Mzee kiongozi wa kanisa, mwanamke ambaye alikuwa na umri wa takribani miaka 90, alisema, “Tunarudisha zaka, kwa hiyo inakulazimu kuhubiri.” Kwa hiyo nilihubiri. Hubiri langu lilitoka katika kitabu cha Yohana 15:4–8. Katika aya nne Yesu anarudia “Kaeni ndani Yangu” mara tatu. Katika utamaduni wa Kiebrania, jambo linaporudiwa mara tatu ni muhimu sana yaani muhimu mno. Nilisisitiza kwamba cha muhimu sana si kile tunachokifanya katika maisha ya Kikristo. Tunapoitwa kutumika, hatuwezi kuwa na matokeo kwa uwezo wetu wenyewe. Hata hivyo Yesu alitoa Neno Lake kwamba ikiwa tutadumu kukaa ndani Yake, chochote tutakachoomba, tutatendewa. Hakuna utata; ni uthibitisho wa mafanikio kwa asilimia 100. “Kwa hiyo,” niliwaambia wasikilizaji, “si kile tunachofanya kiletacho mabadiliko, bali kile ambacho Mungu anaweza kufanya.” Mwandishi Ellen G. White anaeleza, “Si uwezo ulio nao sasa, au utakaowahi kuwa nao, utakaokupa mafanikio. Ni yale ambayo Bwana anaweza kufanya kwa ajili yako. Tunahitaji kuwa na imani kidogo mno katika kile ambacho mwanadamu anaweza kufanya, bali kuwa na imani zaidi katika kile ambacho Mungu anaweza kufanya kwa kila nafsi inayoamini” (Christian Service, uk. 262). Niliwaambia kusanyiko langu dogo kwamba maombi “ni siri ya kuwa na nguvu za kiroho” (Prayer, uk. 12). Yanatuunganisha na (Chanzo cha nguvu” (Steps to Christ, uk. 95). Ni silaha yenye ufanisi zaidi dhidi ya mashambulizi ya Shetani (Testimonies for the Church, vol. 1 uk. 295, 296, 345, 346). Niliwaambia juu ya ahadi ambayo Yesu aliitoa katika Mathayo 18:19, 20. “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Haisemi “ikiwa 200 au 300 wataomba” bali “ikiwa 2 au 3 wataomba” kwa ajili ya jambo fulani kwa mapatano, katika umoja. Na sio “Ninaweza nikalifanya” bali kwa uwazi kabisa “Nitalifanya.” Niliwaambia wasikilizaji wangu wachache, “hatuwezi kuchagua kutofanya kitu. Lazima tuombe na kufanya kazi, kisha Mungu ataleta matokeo kama alivyoahidi.” Lilikuwa hubiri bora juu ya nguvu ya maombi. Tulipokuwa tukirudi nyumbani, nilimwambia mke wangu, “Tunahitaji kuhama. Hakuna tumaini la ukuaji au kwa kweli wa kitu chochote katika kanisa hili.” Alinikumbusha hubiri langu, kwa ahadi ya Yesu, na kisha akaniuliza, kwa nini usiwaite katika maombi?” Nilisita kufanya hivyo. Wale wanawake wachache walikuja kila asubuhi saa 12:30 asubuhi. Ili kuomba pamoja kwa ajili ya Roho Mtakatifu, ukuaji wa kanisa, familia, jiji, mpango wa Mungu kwa kanisa letu na uwazi kwa kile tunachotaka kukifanya. Miezi mitatu baadaye kanisa lilikuwa na watu waliohudhuria takribani 120. Mungu anakuita ili udumu ndani Yake, omba bila kukoma, baki ukiwa umeunganishwa na kutembea Naye. Anakualika ukae ndani Yake, na lazima kila siku umkaribishe akae ndani yako. Hicho ndicho chanzo chako pekee cha nguvu ya kweli. Huo ndiyo usalama wako. Maadamu umeunganishwa na Mungu, Shetani hana nguvu juu yako. Kristo ndani yako na wewe ndani Yake ni njia moja ya kukua na kufanikiwa. Mapendekezo ya Nyimbo Nyimbo za Kristo: • Kaa Nami (19 Vk & 91 Vd) • Ni Wako Bwana (159 Vk & 144 Vd) • Moyoni (400 Vk & 211 Vd) LINK:    • SIKU 10 ZA MAOMBI 2025 || SIKU YA 1 || KAE...   SHARE | SUBSCRIBE | LIKE | COMMENT