ONYO ZITO: JAJI MKUU AFICHUA KINACHOCHELEWESHA KESI MAHAKAMANI "HAKI INACHELEWA!"
HARAKATI TV
0:00 / 0:00
ONYO ZITO: JAJI MKUU AFICHUA KINACHOCHELEWESHA KESI MAHAKAMANI "HAKI INACHELEWA!"
17 504 просмотра · Трансляция закончилась 4 часа назад
HARAKATI TV
97,1 тыс. подписчиков
17 504 просмотра · Трансляция закончилась 4 часа назад
ONYO ZITO: JAJI MKUU AFICHUA KINACHOCHELEWESHA KESI MAHAKAMANI "HAKI INACHELEWA!"
Hotuba ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju wakati wa kufunga Mkutano wa Wadau kuhusu Ushirikiano na Mahusiano katika Utelekezaji wa Majukumu ya Utoaji Haki Mahakamani, uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2026 Makao Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania Dodoma.
JAJI ANASEWMA “Kwa hiyo, mahakama haiwezi kuwa na ufanisi wa asilimia mia moja ikiwa hatua zilizotangulia za mnyororo wa haki jinai hazijafanyika mapema, ipasavyo na kwa ufanisi.
Tunaweza kuwa na mahakama yenye uwezo wa kusikiliza mashauri, majaji na mahakimu wenye uwezo, mifumo ya kielektroniki na miundombinu, lakini pia tukawa na watu waadilifu.
Lakini kama uchunguzi haujakamilika, jalada halijawasilishwa, mashahidi hawapatikani, vielelezo havijakamilika, hati za mashtaka hazijakamilika, mshtakiwa hajaletwa mahakamani au nyaraka muhimu hazijafikishwa mahakamani mapema, katika mtiririko kama huu kesi haiwezi kwenda mbele.
Hata kama kukawa na ile systematic flow ya criminal justice, yaani mfumo wa mtiririko wa haki jinai wa case management, bado kesi haiwezi kwenda mbele kama hatua hizo za awali hazijakamilika.”
Usisahau ku-subscribe Harakati TV, kubonyeza kengele ya taarifa na kushiriki video hii ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
#TunduLissu #Lissu #CDFMkunda #IGPWambura #DCIKingai #Chadema #KesiYaUhaini #Mahakama #Tanzania #HarakatiTV