Перейти к содержимому

CRDB YAZINDUA MKOPO UGHAIBUNI YATENGA BILIONI 250

TimesMajira Tv

0:00 / 0:00

CRDB YAZINDUA MKOPO UGHAIBUNI YATENGA BILIONI 250

66 просмотров · 6 дней назад
TimesMajira Tv
8,31 тыс. подписчиков
66 просмотров · 6 дней назад
BENKI YA CRDB YAZINDUA MKOPO UGHAIBUNI KUWEZESHA WANAOENDA KUFANYA KAZI NJE NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Wilbard Munisi, amewataka vijana wanaopata fursa za ajira nje ya nchi kutumia mikopo inayotolewa na Benki ya CRDB ili kukabiliana na gharama za maandalizi ya safari na kuweza kutimiza ndoto zao za kiuchumi. Dkt. Munisi ametoa ushauri huo leo Agosti 27, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Mkopo wa Ughaibuni, unaolenga kuwawezesha Watanzania waliopata ajira nje ya nchi kugharamia mahitaji muhimu kabla ya kuanza kazi. Amesema mpango huo utawanufaisha hususan vijana wenye sifa na waliopata nafasi za ajira nje ya nchi, lakini wanakabiliwa na changamoto ya kushindwa kumudu gharama za awali kama vile kupata hati ya kusafiria, vibali vya kazi na nauli ya ndege. Akizungumza na mawakala wanaoshughulika na kuwapeleka Watanzania kufanya kazi nje ya nchi, Dkt. Munisi amewataka kuhakikisha wanawaelekeza vijana wenye sifa zinazohitajika kwenye taasisi za fedha ili kupata mikopo badala ya kusafiri bila maandalizi ya kutosha. “Mawakala mnaopeleka vijana kufanya kazi nje ya nchi, hakikisheni wale wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama mnawaleta CRDB wakiwa na vigezo vinavyohitajika, ikiwemo barua ya mwajiri, ili wapatiwe mikopo kwa riba nafuu na nao wafikie ndoto zao. Msiwasafirishe nje kiholela bila kuwa na akiba ya fedha,” amesisitiza. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manunuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema benki hiyo imetenga Shilingi bilioni 250 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wanaotamani kufanya kazi nje ya nchi kumudu gharama za maandalizi ya safari. Amesema kupitia Mkopo wa Ughaibuni, vijana watakaokuwa wamepata ajira nje ya nchi wataweza kupata mkopo wa kuanzia Shilingi 500,000 hadi Shilingi milioni 20, kulingana na vigezo na mahitaji yao. “Kama kijana yupo tayari kwenda kufanya kazi nje ya nchi, sisi tupo tayari kumwezesha ili asikwame kupata vibali vya kazi, hati ya kusafiria na nauli ya ndege. Tunakopesha kuanzia Shilingi 500,000 hadi Shilingi milioni 20, lakini anatakiwa kuwa na akaunti ya Tanzanite,” amesema Philemon. Aidha, amesema mnufaika wa mkopo huo atapewa kipindi cha neema cha miezi miwili baada ya kuanza kazi, kabla ya kuanza kurejesha mkopo wake kidogokidogo kupitia akaunti ambayo mshahara wake utakuwa ukiingizwa. Mpango huo unatarajiwa kuwa suluhisho kwa baadhi ya changamoto zinazowakabili vijana wanaopata fursa za ajira nje ya nchi lakini kushindwa kuzifikia kutokana na ukosefu wa fedha za kukamilisha maandalizi muhimu ya safari. Mkopo huo pia unatarajiwa kuongeza fursa kwa vijana wengi kupata ajira, kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.