JIHAN DIMACK APEPELUSHA BENDERA YA TANZANIA MISS GRAND INTERNATIONAL #caldera tv#Tanzania
CALDERA TV
0:00 / 0:00
JIHAN DIMACK APEPELUSHA BENDERA YA TANZANIA MISS GRAND INTERNATIONAL #caldera tv#Tanzania
751 просмотр · 12 дней назад
CALDERA TV
144 подписчика
751 просмотр · 12 дней назад
Tanzania kupitia mrembo wake Jihan Dimack, imeingia katika hatua ya pili ya kipengele cha Country’s Power of the Year katika mashindano ya Miss Grand International 2026. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Miss Grand International imetangaza makundi manne ya washiriki 40, ambapo Tanzania imepangwa katika Kundi A, likiwa na nchi nyingine tisa, zikiwemo Chile, Indonesia, Mexico, Peru na Uingereza.
Jihan Dimack ni mrembo mwenye asili ya Tanzania na Lebanon, aliyewahi kutwaa taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2016 na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Universe yaliyofanyika Ufilipino mwaka 2017. Kwa sasa, anafanya kazi katika sekta ya uanamitindo, mauzo na utangazaji wa bidhaa, huku akitumia uzoefu wake wa kimataifa kuitangaza Tanzania katika jukwaa la urembo duniani.
Kwa wa mujibu wa taarifa ya grand international upigaji kura wa raundi ya pili umeanza Septemba 28, 2026, saa 5:00 usiku kwa saa za africa mashariki na unatarajiwa kufungwa Septemba 30, 2026, saa 5:00 usiku.
Washiriki wawili pekee kutoka kila kundi watasonga mbele kwenda hatua inayofuata. Upigaji kura unafanyika kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Miss Grand International, ambapo alama zinahusisha asilimia 95 ya wafuasi wapya na asilimia 5 ya ushiriki kupitia like comment na share
Watanzania kwa ujumla wanahimizwa kumuunga mkono Jihan Dimack kwa kumfuatilia kupitia ukurasa rasmi wa Miss Grand International na kushiriki katika upigaji kura kwa kufuatal masharti yaliyowekwa.
Ushiriki huo unalenga kumsaidia mrembo huyo kuendelea na hatua zinazofuata za mashindano hayo ya kimataifa, huku akiibeba bendera ya Tanzania katika jukwaa la urembo na utamaduni duniani.
#missworld2026
#jihan Dimack
#Tanzania