Перейти к содержимому

MAKALLA AZIVALIA NJUGA KERO YA BARABARA NA TEMBO LIWALE

COM MEDIA

0:00 / 0:00

MAKALLA AZIVALIA NJUGA KERO YA BARABARA NA TEMBO LIWALE

321 просмотр · 1 год назад
COM MEDIA
5,79 тыс. подписчиков
321 просмотр · 1 год назад
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema katika Wilaya ya Liwale mkoani Lindi wananchi wanachangamoto kubwa ya barabara, wanyamapori pamoja na umeme unaosababisha kukwama kwa shughuli za kiuchumi katika wilaya hiyo. Makalla ameeleza hayo leo Aprili 11,2025 wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Makalla amesema ili kuweza kutatua changamoto hizo mawaziri wa wizara husika akiwemo Waziri wa Ujenzi na Maliasili na Utalii kufika katika Wilaya hiyo ili kuona namna wanaweza kusaidia utatuzi wa changamoto hizo katika wilaya hiyo. Akitoa ufafanuzi juu ya changamoto za wananchi wa Wilaya hiyo Makalla alimtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana kufika katika Wilaya hiyo ili aweze kuona namna wanaweza kutatua changamoto hiyo ya Tembo katika Wikaya ya Liwale kwani wanyama hao ni hatari na wanasababisha vifo kwa wananchi. “Mheshimiwa Mbunge ameeleza amesema kuhusu TANAPA amesema TAWA nimemwambia walifanya kazi juzi namna walivyofanya kitaalamu kusogeza na kudhibiti Tembo katika maeneo mbalimbali, nimemtaka waziri mwenyewe na timu yake waje hapa Liwale mumpokee mumueleze vizuri,” amesema Makalla. Akizungumza na wananchi hao kwa njia ya simu Ulega alisema kuwa katika bajeti atakayoisoma katika wiki mbili zijazo aliwahakikishia kuwa barabara hiyo itakuwa ni moja wapo kuanzia Nangurukuru mpaka Liwale yenye umbali wa kilometa 231 na kutoka Liwale hadi Nachingwea ambayo itakuwa na kilometa 50 za kuwekwa lami kutokana na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.