Перейти к содержимому

NGUVU YA IMANI NYAKATI ZA MWISHO | SEHEMU YA 1

RGC MINISTRY

0:00 / 0:00

NGUVU YA IMANI NYAKATI ZA MWISHO | SEHEMU YA 1

670 просмотров · 5 л. назад
RGC MINISTRY
69,1 тыс. подписчиков
670 просмотров · 5 л. назад
Tunaishi katika nyakati za mwisho. Imani za wengi zinajaribiwa. Bila kujalisha wewe ni nani, ila upo kati ya viwango hivi vitatu vya imani. Mosi, kiwango cha kutokuwa na imani kabisa. Marko 4:40. Pili, kiwango cha imani chache/haba. Mathayo 6:30, 8:26, 14:31. Tatu, kiwango cha imani KUBWA. Mathayo 8:10, 15:28. Imani katika Kristo Yesu ni matokeo ya kusikia neno la Mungu (Warumi 10:17). Kadiri unavyosikia neno la Mungu na kulitenda ndivyo unaimarisha imani yako na kuikuza. Bila kujalisha nafasi uliyonayo katika Kristo Yesu utakutana na majaribu kutoka kwa shetani, kama huna msingi imara wa neno la Mungu huenda ukashindwa. Kwa sababu hii, jenga imani yako katika neno la Mungu ili mafuriko na dhoruba zikujiapo uwe thabiti kukabiliana nazo. Ikumbukwe kuwa Yesu yu karibu kuja kulichukua kanisa lake (mimi na wewe) na jambo mojawapo atakaloliangalia ni IMANI. Biblia inasema, "walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?" Luka 18:8. Imani ni kito cha thamani kinachopaswa kulindwa kila uchao na kila aliye na safari ya kwenda mbinguni. Hii haitamsaidia tu kwenda mbinguni bali hata kuishi kwa kumpendeza Mungu awawapo duniani .Waebrania 11:6. Vilevile kupitia imani, mwamini atapata mahitaji yake toka kwa Mungu. Nikupe shauri leo, amua kujifunza kwa kina kuhusu Kristo Yesu BWANA kwa kusikiliza mafundisho haya, kusoma Biblia wewe binafsi na zaidi kuyaweka katika matendo. Hakikisha unasikiliza na sehemu ya pili ya somo hili ili ujifunze kwa undani zaidi. Wasiliana nasi kwa: SIMU: +255 764 711 544 E-mail: rgcm0717@gmail.com Youtube:    / rgcmtv​   Facebook:   / rgcministry   Instagram:   / rgcministry   Online Redio: https://www.beaconradi.airtime.pro. SADAKA M-PESA +255 (0) 764 711 544 CRDB BANK ACC.NO: 0152236827400 (JINA:DANIELY JACKSON MREMA. MUNGU AKUBARIKI SANA.