Перейти к содержимому

WAZIRI MKUU AKEMEA VIKALI VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

MEC DIGITAL TV

0:00 / 0:00

WAZIRI MKUU AKEMEA VIKALI VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

92 просмотра · 4 дн. назад
MEC DIGITAL TV
21 подписчик
92 просмотра · 4 дн. назад
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuvielekeza vyombo vya dola kuchukua hatua stahiki wa yoyete atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo. . Mwigulu Dkt Mwigulu Nchemba ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wabunge wa Mkoa wa Ruvuma, jijini Dodoma kufuatia vurugu zilizotokea hivi karibuni baina ya wakulima na wafugaji, zilizosababisha madhara mbalimbali vikiwemo vifo. Kufuatia tukio hilo na mengine yanayoendelea kutokea maeneo mbalimbali Nchini Waziri Mkuu amewaagiza viongozi katika ngazi za vijiji hadi kata kuhakikisha uuzaji na ugawaji wa ardhi unazingatia miongozo, kanuni na sheria za matumizi bora ya ardhi Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Serikali haivumilii vitendo vya uvunjifu wa sheria na amewataka wananchi kuheshimiana, kuvumiliana na kuzingatia sheria katika kutekeleza shughuli zao za kiuchumi. Dkt Mwigulu amesema Serikali haiungi mkono uchukuaji wa sheria mkononi, na vitendo hivyo ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi, hivyo kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zilizowekwa na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza wajibu wake. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru na Watanzania wote walioathiriwa na matukio hayo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na makosa hayo. Pia, Waziri Mkuu ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda tunu za Taifa, hususan amani na mshikamano, uliyoasisiwa na wazee wetu Mwisho