Перейти к содержимому

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS | 18 SEPTEMBER 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

0:00 / 0:00

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS | 18 SEPTEMBER 2026

8 977 просмотров · Трансляция закончилась 10 ч назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
64,5 тыс. подписчиков
8 977 просмотров · Трансляция закончилась 10 ч назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS | 18 SEPTEMBER 2026 UJUMBE WA LEO: PANUA MAHALI PA HEMA YAKO (ENLARGE THE PLACE OF YOUR TENT) Isaya 54 : 2 - 3 2 Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. 3 Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu. KUJAALIWA NA MUNGU! 1 Nyakati 4 : 10 10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba. Mungu ndiye anayemjalia mtu yale anayoyaomba, hivyo unapoomba kwa habari ya kupanua mahali pa hema yako amini tu kwamba Mungu atakujalia hivyo. 1.OMBA TOBA KWA AJILI YA MAHALI PA HEMA YAKO UNAPOTAKA MUNGU APAONGEZE. (NDOA, BIASHARA, KARAMA, KIPAWA, TAALUMA,MASHAMBA, MIFUGO) Zaburi 103 : 8 - 9 8 Bwana amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. 9 Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika hasira yake milele. 2. OMBEA HALI YA KIROHO YA ENEO ULILOPO ISIZUIE KUPANUA MAHALI PA HEMA YAKO. 2 Wafalme 2 : 21 21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. 3.VUNJA ROHO ZOTE ZINAZOKUZUIA KUPANUA MAHALI PA HEMA YAKO (MAGONJWA, UMASIKINI, KUKATALIWA/KUSAHAULIWA, UTASA, UKAUFU) 1 Yohana 3 : 8b 8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. OMBI MAALUMU KWA VIJANA OMBEA MAONGEZEKO YA NDANI (CAREER DEVELOPMENT) Mwanzo 30 : 43 43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda. Mhubiri: Andrew Bartimayo Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com