MUNGU WA MIUJIZA HAYUPOGO TENA. NINI TUFANYE?
Festo Michael Kambarangwe - Official
0:00 / 0:00
MUNGU WA MIUJIZA HAYUPOGO TENA. NINI TUFANYE?
8 просмотров · 7 дн. назад
Festo Michael Kambarangwe - Official
23 подписчика
8 просмотров · 7 дн. назад
Katika kipande hiki cha Dibaji (Segment 2, Cut 3), tunaweka wazi mjadala mzito kuhusu changamoto yetu kuu ya maendeleo: uwepo wa uhafidhina na wahafidhina miongoni mwetu — lakini je, ni wahafidhina wa aina gani?
Mara nyingi tunawatazama wahafidhina wa kisiasa kwa sababu wapo wazi zaidi. Lakini vipi kuhusu wahafidhina katika akademia, madhabahuni, elimu za jadi na za kiroho? Hawa ndio wenye mamlaka ("agency"), ushawishi ("muscles"), elimu na maamuzi yanayotufunga akili na yanayogusa maisha yetu ya kila siku. Hatari ni kama wamefunga akili zao na zetu ndani ya boksi la mazoea, wakikataa kubadilika wala kuamini katika mapinduzi ya kifikra.
Huu ni mwaliko wa kujitathmini kwa kina:
• Nani wanufaika na wenye nguvu (muscles & agency) katika mfumo huu wa uhafidhina?
• Vipaumbele vyetu: Kwanini tunamwaga mamilioni kwenye "bata", kitchen party, na starehe huku elimu, sayansi, na tafiti vikikosa msukumo?
• Somo la Hamza Kalala: Je, kulewa umaarufu wa muda mfupi kunatupofusha kujenga misingi halisi na endelevu?
• Kuangusha mibuyu na majiti makubwa: Je, vipaumbele vyetu na maamuzi yetu ni salama kwa nyumba, miundombinu, shule, na mazingira ya wanetu, na hatma zetu?
• Ukweli mgumu: Mungu wa miujiza hayupogo tena kwa mtindo wa kale wa kuingilia kati kila saa ("Management by walking around"). Mungu keshasimika sheria asilia (laws of nature), mifumo ya kiutawala (kisoftware), na kampa mwanadamu akili na uhuru.
Hatma yetu haiko kwenye kusubiri miujiza jangwani—uamuzi wa kusuka au kunyoa uko mikononi mwetu wenyewe.
📌 TIMESTAMPS:
00:00 - Uliberali uliokithiri na mitego ya fikra
00:15 - Wahafidhina: Mazao ya elimu ya darasani, jadi, na kiroho
01:28 - Wahafidhina wa akademia na imani dhidi ya wale wa kisiasa
02:18 - Wenye mamlaka ("muscles & agency"): Kwanini hawaoni nje ya boksi?
03:15 - Mfano wa Wana wa Israeli: Je, tumekwisha fika Kanaani?
04:46 - Ukweli mgumu: Mungu wa miujiza hayupogo tena
05:56 - Mungu kashamaliza kazi: Kuweka sheria asilia (laws of nature) badala ya MBWA
07:21 - Vipaumbele vyetu: Bongo Flava, brand ambassadors, na role models wa wanetu
07:54 - Swali la kuangusha mibuyu: Je, ni salama kwa nyumba, miundombinu, na shule?
08:55 - Fundisho la Hamza Kalala: "Kujenga jamii haihitaji umaarufu"
09:43 - Mungu katupa akili na uhuru wa kujiongoza (Rejea: Joel 2:28)
10:55 - Kitchen party na starehe vs michango ya elimu na jamii
12:08 - Ugatuzi wa Mungu: Uongozi wa kisoftware na mifumo
12:48 - Uamuzi wa kusuka au kunyoa uko mikononi mwetu wenyewe
🙏 Tafadhali Subscribe, Like, na Share ujumbe huu ili kukuza mbegu za fikra huru na uamsho wa jamii yetu.
#FikraMpya #MunguWaMiujiza #ElimuTanzania #VipaumbeleVyetu