Перейти к содержимому

“MSITUJARIBU!” TUMEKOSA NINI HADI MTULETEE POLISI NA MABUNDUKI?

TMC NEWS TV

0:00 / 0:00

“MSITUJARIBU!” TUMEKOSA NINI HADI MTULETEE POLISI NA MABUNDUKI?

13 613 просмотров · 2 дн. назад
TMC NEWS TV
42,5 тыс. подписчиков
13 613 просмотров · 2 дн. назад
Wafanyabiashara wa machinga waliokuwa wakifanya biashara eneo la One Way jijini Dodoma wameeleza changamoto wanazokabiliana nazo katika kutafuta maeneo ya kufanyia biashara baada ya kuondolewa katika maeneo yao ya awali. Machinga hao wanasema wamewasilisha malalamiko na mapendekezo yao kwa viongozi mbalimbali wakitarajia kupata suluhisho, lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya kupata eneo linalowawezesha kuendelea na shughuli zao za kujipatia kipato. Wamehoji sababu ya kuletwa kwa polisi na askari wenye silaha wakati wakijaribu kutafuta suluhisho, wakisisitiza kuwa wanachohitaji ni nafasi ya kufanya biashara na kutunza familia zao, si kugombana na mtu yeyote. Baadhi yao wamesema wamekaa takribani miezi miwili bila kufanya biashara na sasa wanaiomba Serikali kuwasikiliza, kuzingatia mapendekezo yao ya maeneo mbadala na kutafuta suluhisho linalozingatia hali zao za kiuchumi. Hata hivyo, TMC NEWS haikushuhudia uwepo wa polisi katika eneo hilo wakati wafanyabiashara hao wakieleza malalamiko yao. Je, una maoni gani kuhusu kilio cha machinga wa One Way jijini Dodoma? Tuandikie kwenye sehemu ya maoni (COMMENT). NEWS | Shaping The Future Asante kwa kufuatilia TMC NEWS. Subscribe, Like na Share ili kuendelea kupata habari za uhakika, matangazo ya moja kwa moja na uchambuzi wa kina kutoka Tanzania na duniani. 🔔 Washa arifa (Notifications) ili usipitwe na taarifa muhimu. 📢 Kwa matangazo, ushirikiano na maoni: 📧 tmcnewsmedia@gmail.com 📞 +255 674 075 414 🌐 Tufuatilie kwenye mitandao yote ya kijamii: @tmcnewsmedia #TMCNews #ShapingTheFuture #BreakingNews #TanzaniaNews #LiveNews#TMCNews #Machinga #MachingaWaOneWay #OneWayDodoma #Dodoma #DodomaCity #MachingaDodoma #Biashara #Wafanyabiashara #HakiZaMachinga #ChangamotoZaMachinga #MachingaComplex #Tanzania #HabariZaTanzania #BreakingNews #TaarifaZaHabari #HabariLeo #SautiYaWananchi #WananchiWanasema #Ajira #Vijana #Ujasiriamali #BiasharaNdogo #Serikali #ShapingTheFuture