WATUHUMIWA 9 WAKAMATWA KWA MAUAJI YA MWANAFUNZI PEMBA
MJAWIR MEDIA
0:00 / 0:00
WATUHUMIWA 9 WAKAMATWA KWA MAUAJI YA MWANAFUNZI PEMBA
3 793 просмотра · 1 день назад
MJAWIR MEDIA
16,2 тыс. подписчиков
3 793 просмотра · 1 день назад
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limewatia mbaroni watuhumiwa tisa (9) kuhusiana na tukio la kinyama la mauaji ya mwanafunzi Raiyan Hemed Amour, mwenye umri wa miaka 15.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo ulipatikana katika kichaka huko kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, ukiwa umekatwa kiganja cha mkono wa kulia kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Ukamataji huu umefuatia doria na msako mkali ulioanza tangu Septemba 23 na kuendelea kisiwani humo. Polisi wamehakikisha kuwa uchunguzi bado unaendelea na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika pindi uchunguzi utakapokamilika.