MAHAKAMA YAAMURU MZEE KULIPWA MIL. 100 NA MITANDAO YA SIMU KISA KUFUNGA KWA LAINI ZAKE
Bongofive Plus и Bongo5
0:00 / 0:00
MAHAKAMA YAAMURU MZEE KULIPWA MIL. 100 NA MITANDAO YA SIMU KISA KUFUNGA KWA LAINI ZAKE
8 330 просмотров · 12 дней назад
Bongofive Plus и Bongo5
8 330 просмотров · 12 дней назад
MAHAKAMA IMEAMURU NILIPEWE ZAIDI YA MILIONI 100, LAKINI HADI SASA SIJAONA FEDHA”
Mzee Anney Safari Anney amesafiri kutoka Arusha hadi Dodoma kufuatilia malipo baada ya kushinda shauri la kudai kurejeshewa laini zake za simu zilizofungwa baada ya kushindwa kusajili kwa alama za vidole.
Anney amesema alishindwa kusajili laini hizo kutokana na vidole vyake kulika baada ya kutumia kwa muda mrefu kuendesha baiskeli ya miguu mitatu.
Amesema Mahakama imeamuru mitandao hiyo ya simu kumlipa zaidi ya Shilingi milioni 100 kama fidia, ikiwemo gharama na usumbufu alioupata katika kipindi cha miaka minne aliyokaa Dodoma akifuatilia shauri hilo.
Mzee Anney ameishukuru Mahakama kwa uamuzi huo, lakini amesema hadi sasa hajapokea fedha hizo, hali inayomfanya aendelee kuishi maisha magumu.
Amesema baadhi ya watu wanaomdai wamekuwa wakidhani tayari amelipwa baada ya kusikia kuwa Mahakama imetoa uamuzi wa kumlipa zaidi ya Shilingi milioni 100.