Перейти к содержимому

Kutoka Cherehani Moja Hadi Kiwanda Kinachosambaza Kariakoo | BoEn Show

Mawo Buy

0:00 / 0:00

Kutoka Cherehani Moja Hadi Kiwanda Kinachosambaza Kariakoo | BoEn Show

100 просмотров · 1 дн. назад
Mawo Buy
585 подписчиков
100 просмотров · 1 дн. назад
Alianza kwa kushona nguo moja moja. Leo ana kiwanda kinachosambaza Kariakoo. 🧵 Katika episode ya kwanza ya BoEn Show, tunamtembelea Beatrice, mmiliki wa kiwanda cha nguo na Adrice Collection, ndani ya kiwanda chake. Anatueleza kila kitu kwa uwazi: alivyoweka akiba kila shilingi alipokuwa akifanya kazi za modeling Japan, alivyojipa miezi sita kujaribu wazo lake, changamoto za mafundi na wateja, na kwa nini anaamini kwamba hata akipoteza kila kitu, hajapoteza chochote. 📌 UTAJIFUNZA: Jinsi ya kujenga mtaji bila kuomba mkopo Kwa nini nidhamu ni muhimu kuliko kipaji Siri ya pattern za karatasi inayozuia hasara kiwandani Namna ya kumhudumia mteja mwenye hasira Kwa nini quality lazima iendane na bei Unachofanya siku unayotaka kukata tamaa ⏱️ CHAPTERS 0:00 Utangulizi 0:42 Karibu kiwandani 1:19 Alianzaje? Kutoka mwanamitindo hadi fundi 2:01 Akiba ya Japan: mtaji wa kiwanda 4:31 Mashine kubwa vs butterfly: siri ya quality 5:43 Kutoka fundi hadi mfumo: utafiti wa kuanzisha kiwanda 7:03 Kiwanda kinazalisha nguo ngapi kwa siku? 8:00 Watanzania na "nguo special" 9:13 Kwa nini mizigo huchelewa? 11:49 Malipo na ubora wa kazi 14:11 Kurudi Tanzania: changamoto ya material 16:12 Tracksuit ya kwanza ya kitambaa cha sababi 19:07 Kuongoza wafanyakazi wenye akili tofauti 22:16 Changamoto za mafundi wa Kitanzania 24:28 Nidhamu: somo ambalo shule hazifundishi 24:51 Mteja akija na hasira 25:47 Fundi mwenye kipaji au mwenye nidhamu? 27:13 Pattern za karatasi: jinsi ya kuepuka hasara 30:28 Sheria za kiwanda 31:46 Siku unazotaka kukata tamaa 33:58 Kitu kimoja angebadilisha kwenye tasnia 35:13 Akipoteza kila kitu, angefanya nini? 💬 SWALI KWAKO: Ungechagua nani kiwandani kwako: fundi mwenye kipaji kikubwa lakini nidhamu ndogo, au fundi wa kawaida mwenye nidhamu ya juu? Tuambie kwenye comments 👇 👤 MFUATILIE BEATRICE: Instagram @beatrice_only1 🎬 KUHUSU BoEn SHOW BoEn (Born Entrepreneur) ni kipindi kinachoandika hadithi halisi za wajasiriamali halisi wa Tanzania na Afrika Mashariki: changamoto zao, maamuzi yao na masomo yao. BoEn by Mawo. 🔔 Subscribe na bonyeza kengele usikose episode inayofuata. #BoEnShow #Ujasiriamali #BiasharaTanzania