Перейти к содержимому

Safari ya Imani(Official video)

St. Anthony Cathedral Choir Malindi

0:00 / 0:00

Safari ya Imani(Official video)

88 362 просмотра · 1 год назад
St. Anthony Cathedral Choir Malindi
38,2 тыс. подписчиков
88 362 просмотра · 1 год назад
SAFARI YA IMANI OFFICIAL VIDEO BY ST. ANTHONY CATHEDRAL CHOIR MALINDI SAFARI YA IMANI 1. Safari ya Imani ni ndefu (na) ilianza tangu kale, Manabii walitembea (kweli), wakiwa na Imani, Makuhani na wahudumu (pia) waliomba Imani, Mitume wa Yesu wakaja (nao) wakaleta Imani, Mashahidi wa Uganda Karoli Lwanga na wenzake wakajazwa Imani thabiti, (kamwe) hawakuogopa moto (hata) kisu wala mkuki, wote (walikufa kishujaa kwenye safari ya Imani x2). {Kwa Imani ninajua kwamba niko salama, safarini naamini nitafika salama, nakaza mwendo sana nifike mbinguni, nikae na wale washindi wa Imani, Bwana naomba niongeze Imani, niwe imara nishinde majaribu x2} 2. Safari ya Imani ni ndefu, (na) njia zote ni nyembamba, Wanadhiri walitembea (kweli) wakiwa na Imani, Mamajusi wenye akili (pia) waliomba Imani, Missionary wote wakaja (nao) wakaleta imani, Mashahidi wa Uganda George Kizito na wenzake wakajazwa imani thabiti, (kamwe) hawakuogopa; moto (hata) kisu wala mkuki, wote (walikufa, kishujaa kwenye safari ya Imani.) x2 3. Safari ya imani ni ndefu (na) mawimbi ni makubwa Watabiri walitembea (kweli) wakiwa na imani, Wafalume na wachungaji (pia) waliomba imani, Mapadiri hata wakaja (nao) wakaleta imani, Mashahidi wa Uganda Mbagga Tuzinde na wenzake wakajazwa imani thabiti, (kamwe) hawakuogopa moto (hata) kisu wala mkuki wote (walikufa, kishujaa kwenye Safari ya Imani.) x2