Перейти к содержимому

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING [ 21 SEPTEMBER 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

0:00 / 0:00

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING [ 21 SEPTEMBER 2026

4 618 просмотров · Трансляция закончилась 18 часов назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
64,6 тыс. подписчиков
4 618 просмотров · Трансляция закончилась 18 часов назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING [ SEPTEMBER 2026 UJUMBE WA LEO : WAKUU WALIOFUNGWA NENO KUU: Isaya 22 : 3 Wakuu wako wote wamekimbia pamoja, Wamefungwa wasiutumie upinde. Wote walioonekana wamefungwa pamoja, Wamekimbia mbali sana. 1. Kila mmoja anao uwezo wa kuwa mtu mkuu kwenye maisha yake. Anayo mbegu ya ukuu kwenye maisha yake. Luka 1 : 15 15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Mathayo 11 : 11 11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. Kwa sasa hakuna dalili yote ya ukuu kwa jinsi ya nje, ila ndani mtu amebeba ukuu. Ndiyo maana hutakiwi kujiangalia sasa na kuhitimisha kwamba hauna ukuu ndani yako. Fikiri habari za Yusufu na Daudi. Kuna makundi mawili ya watu hapa Watu wanaojua wanaukuu ndani yao. Yusufu alijua Watu wasiojua wana ukuu ndani yao. 2. Ulimwengu wa roho unatambua ukuu wa mtu kwa vile ulivyo rohoni na sio mwilini. Waamuzi 6 : 12 12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa. Mambo ya kuzingatia Jizoeshe kuwatazama watu kwa jinsi ya roho na sio kwa jinsi ya mwili. Ukiwatazama kwa jinsi ya mwili utapotea, utauwadharau. 2 Wakorintho 5 : 16 16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. Usiweke tumaini wala usijiwekeze kwa nje, bali jiwekeze ndani yako kuliko na ukuu. 3. Mungu anaweza kumfanya mtu mkuu, kiasi cha kuwazidi na kuwa na heshima mbele ya wakuu. 1 Nyakati 11 : 20 - 21 20 Tena Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa wale watatu; kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua; akawa na jina kati ya wale watatu. 21 Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Mambo ya kutafakari. Pamoja na kwamba kuna watu wakuu sasa, Mungu anaweza kukuinua zaidi ya hao wao wakuu. Ukuu wao hautakiwi kuwa kipimo chako Mungu anaweza kukufanya mkuu kiasi cha kuwa na heshima katikati ya wakuu. Ni mpaka umekuwa na heshima kati ya wakuu, bado hujafika. Waebrania 7 : 4 4 Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara. Mungu anaweza kumfanya mtu mkuu kiasi kwamba mtu hatishiki, hasumbuki mbele ya wakuu. 2 Wafalme 4 : 8, 13 8 Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula. 13 Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? Je! Uombewe neno kwa mfalme, au kwa amiri wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu, Mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe. (2 Kings 4:13 AMP) "Now he said to Gehazi, “Say to her now, ‘You have gone to all this trouble for us; what can I do for you? Would you like to be mentioned to the king or to the captain of the army?’ ” She answered, “I live among my own people [in peace and security and need no special favors].” Muhubiri :Mwalimu, George Mwakabago Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com