NI UHERI BORA KU MWAMINI BWANA (Lyrics) By Bro Rodrigue Banze
Rodrigue Banze
0:00 / 0:00
NI UHERI BORA KU MWAMINI BWANA (Lyrics) By Bro Rodrigue Banze
53 981 просмотр · 5 л. назад
Rodrigue Banze
5,96 тыс. подписчиков
53 981 просмотр · 5 л. назад
Nyimbo za Wokovu
223. NI UHERI BORA KUMWAMINI BWANA
1. Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu kwa wakati
wa ujana wetu, kabla hatujazionja dhambi na
mashaka zinazoharibu roho zetu.
Ni uheri bora kumwamini Bwana Yesu, na kumfuata kila siku. Na ujana wetu ukitukimbia tena, shangwe ya wokovu itabaki.
2. Ni uheri bora kumtii Bwana Yesu kwa wakati wa
ujana wetu. Hivyo tutakuwa na dhamiri safi, njema
kwa maisha yetu yote pia.
3. Ni uheri bora kumtumikia Yesu kwa wakati wa ujana
wetu. Bwana Yesu akumbuka kila tendo dogo,
atalipa kwa neema yake.
4. Ni uheri bora kumngoja Bwana Yesu kwa wakati wa
ujana wetu. Atatuchukua kwake kwa furaha kubwa,
tutakuwa naye siku zote.