Перейти к содержимому

TRA yatoa zabuni ya huduma za stempu za kielektroniki

TBConline

0:00 / 0:00

TRA yatoa zabuni ya huduma za stempu za kielektroniki

154 просмотра · 7 дней назад
TBConline
526 тыс. подписчиков
154 просмотра · 7 дней назад
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa wito kwa kampuni zenye sifa na uwezo unaohitajika kujitokeza na kuwasilisha maombi ya zabuni kwa ajili ya kutoa huduma za Stempu za Kielektroniki (ETS) zinazowekwa kwenye bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa. Huduma hiyo inalenga kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa, kudhibiti matumizi ya stempu bandia, kupunguza mianya ya ukwepaji kodi na kusaidia kudhibiti bidhaa zinazozalishwa au kuingizwa nchini kinyume cha taratibu. TRA imezihimiza kampuni zenye sifa kushiriki katika mchakato huo kabla ya dirisha la maombi kufungwa Septemba 15, 2026. Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda, ametoa wito huo Septemba 11, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi bajaji kwa watumishi wa TRA wenye mahitaji maalumu. Amesema TRA inatarajia kupata waombaji wenye uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa gharama nafuu, huku wakisaidia kuimarisha udhibiti wa matumizi ya stempu bandia, kupambana na bidhaa za magendo na kudhibiti bidhaa ambazo hazijafuata taratibu zilizowekwa.