Taratibu Zote za Uchimbaji Madini Lazima Ziheshimiwe//Wachimbaji Wasisumbuliwe-WAZIRI BITEKO
Wazohuru Media
0:00 / 0:00
Taratibu Zote za Uchimbaji Madini Lazima Ziheshimiwe//Wachimbaji Wasisumbuliwe-WAZIRI BITEKO
820 просмотров · 4 года назад
Wazohuru Media
20,1 тыс. подписчиков
820 просмотров · 4 года назад
Waziri wa Madini Mhe Dkt. Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 26 Januari 2022 katika kijiji cha Kakola Wilayani Kahama akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga amewatoa hofu wananchi wenye kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu madai ya fidia ya ardhi, ambapo amesisitiza kuwa serikali inafuatilia kwa karibu kuhakikisha wanapata stahiki zao.
Amesema kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika fursa ya uchimbaji madini kwani sekta hiyo imeendelea kubadilisha maisha ya watu ikiwa ni pamoja na kungeza pato la serikali kutokana na rasilimali hiyo.
Amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye kuomba umiliki wa leseni za uchimbaji huku akiweka msisitizo kwa wachimbaji watakaogundua madini kutoingiliwa kinyume na taratibu na sheria za nchi.