ZIARA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA 2 (WAVULANA) MJI WA BAGAMOYO | 2026
Istiqaama Tanga
0:00 / 0:00
ZIARA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA 2 (WAVULANA) MJI WA BAGAMOYO | 2026
837 просмотров · 5 мес. назад
Istiqaama Tanga
340 подписчиков
837 просмотров · 5 мес. назад
𝗦𝗶𝗸𝘂 𝘇𝗮 𝘂𝘀𝗼𝗻𝗶, 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗳𝘂𝗻𝘇𝗶 𝘄𝗮𝗻𝗮𝘁𝗮𝘇𝗮𝗺𝗮 𝘀𝗶𝗸𝘂 𝘇𝗮 𝗸𝗶𝘀𝗼𝗴𝗼𝗻𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝗯𝗮𝘀𝗵𝗮𝘀𝗵𝗮, 𝘁𝗮𝗯𝗮𝘀𝗮𝗺𝘂 𝗻𝗮 𝗳𝘂𝗿𝗮𝗵𝗮 𝗺𝗼𝘆𝗼𝗻𝗶, 𝘄𝗮𝗸𝗶𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝗺𝘂 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗷𝗶𝗳𝘂𝗻𝘇𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝘂𝗲𝗹𝗲𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗼 𝗻𝗷𝗲 𝘆𝗮 𝗺𝗶𝗽𝗮𝗸𝗮 𝘆𝗮 𝗱𝗮𝗿𝗮𝘀𝗮 !!!
Ziara ya mafunzo ya wanafunzi wa kidato cha Pili (Wavulana) katika mji mkongwe wa kihistoria wa Bagamoyo ilikuwa na lengo la kupanua upeo wao wa maarifa kwa kujifunza historia, utamaduni pamoja na mazingira halisi ya maeneo muhimu ya kihistoria.
Katika ziara hiyo, wanafunzi walipata fursa ya kutembelea magofu ya Kaole Ruins pamoja na bandari ya zamani ya Bagamoyo, ambapo walijifunza historia mbalimbali zinazohusu ustaarabu wa kale, biashara pamoja na mchango wa eneo hilo katika historia ya Afrika Mashariki. Mafunzo hayo yaliwawezesha kuelewa kwa kina urithi wa kihistoria na kitamaduni wa Bagamoyo.
Aidha, wanafunzi walitembelea eneo la hifadhi lililopo Kaole na kupata nafasi ya kujionea wanyama mbalimbali pamoja na mazingira ya asili, jambo lililoongeza uelewa wao kuhusu uhifadhi wa mazingira na viumbe hai.
Sambamba na hilo, walipata nafasi ya kutembelea Stone Town, mji wenye historia kubwa na majengo ya kale yanayoakisi mchanganyiko wa tamaduni tofauti. Kupitia ziara hiyo, walijifunza kuhusu maisha ya zamani, usanifu wa majengo ya kale pamoja na nafasi ya mji huo katika historia ya biashara na maendeleo ya Afrika Mashariki. Pia walitembelea soko la zamani na kushuhudia namna shughuli za kibiashara zilivyokuwa sehemu muhimu ya maisha ya kijamii na kiuchumi katika nyakati za kale.
Kwa ujumla, ziara hiyo ilikuwa yenye mafanikio makubwa kwani wanafunzi walijifunza mambo mengi mapya, walipanua upeo wa fikra zao na kupata uzoefu wa kipekee uliowaongezea hamasa katika safari yao ya elimu na maendeleo binafsi.
#WeAreTheReadingUmmah
𝐃𝐞𝐝𝐢𝐜𝐚𝐭𝐞𝐝 𝐭𝐨 𝐄𝐱𝐜𝐞𝐥𝐥𝐞𝐧𝐜𝐞 !
.
.
.
.
.
#IstiqaamaTanga #Istiqaama #Bagamoyo #StudyTour